Claudia Kayombo na Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU Tawala mpya Mkoa wa Singida, Fatma Mganga, amemwomba mkuu wa Mkoa
huu, Peter Serukamba ampe ushirikiano kwani hatakuwa kikwazo kwake.
Fatma ameyasema hayo leo Machi 21,
2023, mkoani hapa wakati wa hafla ya kumkaribisha rasmi, iliyofanyika katika
ukumbi wa mkuu wa mkoa.
“Namshukuru Mungu kwa kuniteua miongoni mwa Watanzania zaidi ya milioni 60
nije Singida. Pili namshukuru sana Rais kwa kuniona, nilikuwa Dodoma sasa
Singida.“Katibu tawala kwa nafasi yake ni mtendaji, naomba ushirikiano wako
mheshimiwa mkuu wa mkoa, naahidi sitakuwa kikwazo kwako, tushirikiane tufanye
kazi vizuri.mkoa upo hivi kutokana na utendaji wenu mzuri,” alisema Fatma.
Hata hivyo, aliwaonya wafanyakazi wa idara mbalimbali kuwa yupo tayari
kupokea maoni siyo majungu, kwani katika maeneo ya kazi majukngu hayana nafasi
kwake.“Mimi kitaaluma ni daktari, niliwahi kuwa mganga mkuu wa wilaya,
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, hivyo, nitawapa
ushirikiano ili kufanikisha yale ambayo Rais anataka yafanyike na akatumia
nafasi hiyo kuwausia wafanyakazi mkoani hapa kumtanguliza Mungu katika kila
jambo.
Kwa upande wake Katibu Tawala aliyemaliza muda wake, Doroth Mwaluko, baada
ya kuwashukuru idara mbalimbali za mkoa huo kwa kufanya nao kazi vizuri ,
alimshukuru mkuu wa mkoa huu, Serukamba kwa kumheshimu wakati wote.
Aidha, Mwaluko aliwasihi wafanyakazi mkoani hapa kufanya kazi kwa weredi
kwani mafanikio ya mkoa yanampa heshima Rais ambaye atazungumzwa vizuri
kutokana na maendeleo ya maeneo husika.
“Watumishi wa umma kazi yetu ni kuwahudumia wananchi, ninyi ni sehemu ya
mafanikio ya Mama Samia, anapotukanwa, kuzungumziwa vibaya ni kwa sababu ya
ninyi, hivyo fanyeni kazi aione ili Rais azidi kutukuka,” alisema Mwaluko.
Akizungumza kwenye mapokezi hayo ya katibu tawala mpya Serukamba aliahidi
kumpa ushirikiano Fatma na akamkaribisha Singida.“Wote ametuleta Rais, nitakupa
ushirikiano, tufanye kazi kwa ufanisi, naombeni sana watumishiwenzangu wa idara
mbalimbali tumpe ushirikiano,
RAS wetu ni mpole lakini anataka matokeo, mimi namfahamu vizuri,” alisema Serukamba.Akimzungumzia RAS mstaafu Mama Doroth alisema alikuwa kiongozi shupavu na hodari, alikuwa akifuatilia mambo mengi serikalini na kuwezesha kutekelezwa miradi mingi ambayo hataile wengine hawakuwa wanaiweza.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mawazo ya mwandishi. 'Hapa ni kama Katibu Tawala aliyemaliza muda wake Doroth Mwaluko (kulia) ana mwambia Katibu Tawala Mpya, Dk.Fatma Mganga kuwa aangalie vizuri jambo aliloliandika hapo kwani lina masilahi makubwa kwa wana Singida hivyo alizingatie'Katibu Tawala mpya Mkoa wa Singida, Dk. Fatma Mganga akisisitiza jambo kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza kwenye hafla hiyo.
0 Comments