NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
PROTOKALI
ni sehemu ya Uhusiano, Balozi (Mstaafu), Mhe. Peter Kallaghe amewaambia Maafisa
Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali (TAGCO) wanaohudhuria Kikao Kazi
cha 18 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)
jijini Dar es Salaam Machi 28, 2028.
Balozi
Kalaghe ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya Protokali (Protocol) kwa
wajumbe wanaoshiriki kikao hicho cha siku tano kilichoanza Machi 27, 2023.
Kazi
ya tasnia yenu ni kufungua milango ambayo imefungwa, tabia ni moja ya njia
bora ya kufungua milango iliyofungwa, alisema.
Aliwaeleza
misingi mbalimbali ya kuzingatia katika Protokali ili kuonyesha ustaarabu
katika ofisi wanazozitumikia.
Baadhi
ya misingi ya Protokali aliyowaeleza Maafisa hao wapatao 600 kutoka Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar, ni dhima ya kuwashauri viongozi wao katika ushiriki
wa matukio mbalimbali ndani ya ofisi na j nje ya ofisi.
Alisema
pamoja na wajibu mwingine Maafisa hao wanawajibu wa kuwashauri viongozi wao kuhusu
kuheshimu mialiko, pia muda, kwani hiyo ni
ishara ya kuonyesha heshima ya shughuli husika .
“
Lazima uonyeshe ustaarabu (etiquette), kwa kujua mambo ambayo kwa utamaduni wa
sehemu fulani linakubalika au halikubaliki.” Alibainisha na kuongeza..
Aliwaeleza
umuhimu wa uchaguzi wa mavazi wanayovaa wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi na
kuwaeleza kuepuka mavazi yanayopiga kelele (shouting collors).
“Unavyovaa
ni sehemu ya weledi wako, kuelewa nguo gani unavaa na kwa wakati gani.”
Alifafanua.
Akieleza zaidi Balozi Kallaghe ambaye ni mbobezi katika fani ya Mawasiliano alisema wanapaswa kujua utaratibu wa ukaaji (Setting arrangement) kwa viongozi wao, namna ya kuzungumza, kutamka majina kwa usahihi.
Balozi (Mstaafu), Mhe. Peter Kalaghe, akizungumza na washiriki.
Balozi Kallaghe akiteta jambo na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sara Kibonde
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao, akiongoza majadiliano.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akijibu baadhi ya hoja za washiriki.
Bw. Kakele na Bw. Msigwa wakiteta jambo
0 Comments