Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akionesha furaha yake katika dua ya hauli ya Sheikh Nassoro Issa Salum Alharith Alqadirii Baba wa Sheikh Issa Nassoro iliyofanyika kwenye Msikiti wa Muhajirina uliopo Majengo Manispaa ya Singida Aprili 7, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro amepiga marufuku wasanii mkoani hapa
kuacha mara moja tabia ya kuchezea alama za dini kwa lengo la kutafuta umaarufu
(kiki)
Nassoro ameyasema hayo wakati akizungumza na Waumini wa dini ya kiislam katika
dua ya hauli ya Sheikh Nassoro Issa Salum Alharith Alqadirii Baba wa Sheikh
Issa Nassoro iliyofanyika kwenye Msikiti wa Muhajirina uliopo Majengo Manispaa
ya Singida Aprili 7, 2023 na baada ya hapo alifuturisha mamia ya waislam
nyumbani kwake futari ambayo ilihudhuliwa pia na viongozi wa juu wa dini hiyo
mkoani hapa.
“Nitoe wito kwa wasanii wa Singida na nje ya Singida kuacha mara moja
michezo ya kutafuta kiki za kuchezea alama za dini niwahusie wasanii wanawake
wafanye usanii wao bila kujishubirisha na wanaume wala na mavazi yao na
halikadharika na wasanii wa Wanaume waache kujishahibisha na wanawake na
walakuvaa nguo zao” alisema Sheikh Nassoro.
Sheikh Nassoro alisema iwapo kutakuwa na ujumbe ambao unatakiwa kufikishwa
kwa wanawake inapaswa watafutwe wao na si watafutwe wanaume na kuwa na hata kwa
wanaume iwe hivyo hivyo na kujimithirisha kuwa mwanamke jambo ambalo
halikubaliki hata kidogo.
Alisema hivi sasa tupo katika mapambano ya kupinga vitendo vya ubaradhuri (ushoga)
lakini tutafanikiwaje kushinda mapambano hayo wakati wanaona kuna wanaume
wanajimithirisha na jambo hilo na kwamba hawakubaliani na vitendo hivyo na
wameiomba Serikali kuliangalia kwa karibu.
Alisema waislam wanalaani sana kitendo kilichoonekana hivi karibuni kwenye
mitandao ya kijamii wanawake wakionekana
wakitangaza biashara huku wakiwa wamevaa kanzu za kiislam kuwa hawakubaliani na
jambo hilo wao wanahesabu kama ni chokochoko dhidi ya waislam na kuwa
wanaiambia Serikali kuwa mwanzo wa uvunjifu wa amani hapa nchini ni masuala
madogomadogo kama hayo.
Sheikh Nassoro alisema wakati vitendo hivyo vikitokea wameibuka baadhi ya
wanasheria wakiwemo waislam ambao wanatetea vitendo hivyo wakieleza kuwa eti wanao
vifanya wana haki ya kufanya hivyo na watahakikisha wanawatetea kuipata hivyo
aliwahimiza waislam kkujitokeza kumuunga mkono Mufti wa Tanzania Sheikh
Abubakar Zubeiry Bin Ali kwenye maandamano ya kupinga vitendo hivyo yatakayo
fanyika kuanzia Msikiti wa Masjid Taqwa hadi Stendi ya Zamani..
Mbunge wa Singida mjini Musa Sima alisema ujumbe mzito alioutoa Sheikh
Nassoro wa kupinga vitendo hivyo unapaswa kuungwa mkono na kuomba Aprili 16,
2023 siku iliyopangwa kufanyika maandamano ya kupinga vitendo hivyo hapa
Singida wananchi wajitokeze kwa wingi.
Aidha, Mbunge Sima alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
na Mkoa wa Singina ukiwa ni mnufaika wa fedha hizo.
Mbunge Sima aliwaomba waislam kutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata
baada ya mwezi huo kuendelea kutenda mema ili Mkoa wa Singida uwe mfano kwa
mikoa mingine.
Sima aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Singida na mikoa mingine kumuombea kwa Mungu Rais Samia ili awe na afya na maisha marefu na kuendelea kuwaongoza watanzania.
Sheikh Nassoro akizungumza na wa umini wa kiislam wakati wa dua hiyo ya kumuombea baba yake.
Vijana wa kiislam wakionesha umahiri wa kuzikiri wakati wa dua hiyo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kulia) akiwa na viongozi wengine wakati wa dua hiyo.
Mwalimu wa dini Isihaka Hassan akitoa mada wakati wa dua hiyo.
0 Comments