Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima, akizungumza na madiwani wa Manispaaya Singida,katika kikao baraza hilokilichofanyika mAY 10, 2023 mjini hapa. Kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Kulanga Kanyanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Mjini, Musa Sima amehimiza madiwani wa Manispaa ya
Singida wawe wanapatiwa taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika
manispaa hiyo jambo litakalo saidia kuifuatilia kwa karibu katika utekelezaji wake.
Sima ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi mjini
hapa jana na kueleza madiwani wanapo julishwa kuhusu miradi hiyo inawasaidia
kuifuatilia kwa karibu zaidi na kutekelezwa kwa ufanisi.
"Serikali chini ya uongozi wa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo hivyo madiwani wanajukumu la kuijua ili waweze kuifutilia katika utekelezaji wake kwani ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo inapotekelezwa miradi hiyo.
Akizunumza katika kikao hicho Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata
aliwataka madiwani kuendelea kusimamia kanuni zote wakati wa vikao vya baraza
hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Kulanga Kanyanga ambaye
ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu alisema Manispaa hiyo itaendelea
kushirikiana na madiwani na wa watumishi wote ili kuipaisha kimaendelea manispa hiyo.














No comments:
Post a Comment