MBUNGE KINGU KUTIKISA JIMBONI BAADA YA VIKAO VYA BUNGE LA BAJETI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, July 3, 2023

MBUNGE KINGU KUTIKISA JIMBONI BAADA YA VIKAO VYA BUNGE LA BAJETI

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akichangia jambo Bungeni.
..................................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu anatarajia kutikisa jimbo hilo mara atakapoanza ziara yake ya kikazi baada ya bunge la bajeti kumalizika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kingu alisema ziara hiyo haitafanana na ziara nyingine  alizowahi kuzifanya kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo hasa baada ya kumalizika kwa bunge la bajeti ambalo alichangia mambo mengi kwa ajili ya maslahi ya wapiga kura wake na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia ziara hiyo, alisema ataifanya katika kata zote kwa kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama chake cha CCM na kufanya mikutano ya hadhara ambapo atasikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na kuwa tayari ratiba ya ziara hiyo amekwisha itoa.

"Katika jimbo la Singida Magharibi Rais Samia Suluhu Hassan mama yetu kipenzi cha watanzania ametufanyia mambo mengi makubwa ya maendeleo tunakila sababu ya kumshukuru na kumuombea kwa Mungu ampe afya na maisha marefu ili aendelee kuongoza nchi yetu," alisema Kingu.

Alitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyotekelezwa katika jimbo hilo ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya cha Sepuka, Ihanja na Igransoni, ujenzi wa barabara, shule za msingi na sekondari, umeme, maji na minara ya simu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa wananchi.

 Kingu akitoa ratiba ya ziara hiyo alisema Julai 11, 2023 ataanza ziara hiyo Kata ya Iyumbu, na Julai 12 atakuwa Kata ya Magungumka na Julai 13 Ighombwe na Julai 25 atakuwa Kata ya Igransoni ambapo Julai 26 atakuwa Ilolo na kumalizia Kata ya Ihanja Julai 25 kwa awamu ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad