Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI) Dkt. Wilson Charles akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Nukta Nundu (BRAILLE) duniani yaliyo fanyika katika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida Februari 22, 2024.
Lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kuhusu haki
za binadamu kwa wenye Ulemavu wa Kuona na Uoni Hafifu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Wasioona Tanzania (TAB), Omari Itambu akizungumza katika maadhimisho hayo.
Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona
Tanzania (TAB), Iddi Damka akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI) Dkt. Wilson Charles akimkabidhi cheti
Kaimu Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF) Mkoa wa Singida, Atufigwege Mwaibasa cha kutambua mchango katika maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu
Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI) Dkt. Wilson Charles akimkabidhi cheti
Meneja wa Tawi la NMB Mkoa wa Singida, Emmanuel Kishosha cha kutambua mchango katika maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa
Singida, Dkt. Fatma Mganga.
(PICHA ZOTE NA SOLOMON PHILEMON)
0 Comments