Mkazi wa Utemini Manispaa ya Singida, Sanje Damiani.
.............................................................
Claudia Kayombo na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
MKAZI wa Utemini, Manispaa ya Singida, Sanje
Damiani (51), (pichani), ambaye anateseka kwa maumivu ya mifupa karibu miaka 40
sasa, anawaomba wasamalia wema popote nchini na hata nje ya nchi yakiwamo
mashirika au taasisi za kidini,
kumsaidia fedha itakayogharamia BIMA kubwa ili akamilishe vipimo
hospitalini ambavyo anashindwa kuvigharamia.
Sanje ambaye kwa sasa anasumbuliwa zaidi na
tatizo la kukakamaa mishipa mkubwa ya shingo linalomfanya ashindwe hata
kuigeuza, uvimbe shingoni na mwili kukosa nguvu, amesema ana amini akipata bima
ataweza kupata matibabu ambayo yatampa nafuu itakayomwezesha kufanya kazi
zitakazomwingizia kipato kuliko sasa ambapo miaka mitatu anaishi kwa kutegemea
huruma ya wasamalia wema.
Akizungumza na waandishi wa habari hii mjini hapa,
Sanje alisema licha ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali tangu akiwa na umri wa
miaka Tisa, yaliyopelekea baadhi ya viungo vya mikono na miguu kufa ganzi hilo
halikumfanya ashindwe kujifunza ushonaji nguo uliokuwa ukimwingiza kipato tangu
alipofika umri wa kuanza kujitegemea.
Akifafanua alisema ni miaka mitatu imepita tangu
uvimbe ulipomwanza shingoni kwa nje baadaye akapatwa na tatizo la kukohoa
mfululizo na hatimaye uvimbe huo uliingia ndani ambapo tatizo la kukakamaa
mishipa ya shingo likajitokeza na kumkalisha chini.
Sanje mama wa watoto wawili ambao wote hawajaanza
kujitegemea alisema alikwenda katika sehemu kadhaa za kutolea huduma za afya
ikiwamo hospitali ya rufaa ya mkoa Singida na Benjamin Mkapa Dodoma, lakini
ameshibdwa kufanyiwa uchunguzi wa kina wa matatizo hayo kwa kushindwa
kugharamia vipimo.
Alibainisha kuwa kwa ujumla kwa sasa anahitaji
msaada wa matibabu, chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu huku akiwashukuru
baadhi ya ndugu zake ambao walimsaidia zaidi kipindi cha mwanzo wakati
changamoto hizo zinamwanza.
Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia kwa namna yoyote, anaweza kuwasiliana naye kwa namba yake ya simu ya mkononi, 0762- 931063 au 0754362990 kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri, shime msaidie mama huyu hata Sh.1000 kwake itakuwa ni kubwa na utapata baraka za Mungu..Mkazi wa Utemini Manispaa ya Singida, Sanje Damiani.akiwa na mtoto wake ambaye anamsaidia shughuli mbalimbali baada ya kutoka shuleni.
0 Comments