Mkuu wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma, akimpanda mti nje ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi Februari 25, 2024.
..........................
Na Issa Mwadangala, Songwe
MKUU wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna
wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian
Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya
Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma mapema leo Februari 25, 2024 alipanda mti
eneo la mbele la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe baada ya kumaliza
ukaguzi wa siku saba wa utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoani humoulioanza
Februari 18 mwaka huu.
Naibu Kamishna MUSHY alifanya ukaguzi na kutoa
mafunzo katika wilaya zote 04 za mkoa wa Songwe ambapo pamoja na kukagua kazi
mbalimbali za Polisi Mkoani humo, pia amefanya vikao kwa nyakati tofauti na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo
mbalimbali.
Aidha katika kikao chake cha majumuisho
alichofanyika tarehe 25 Februari 2024 amewapongeza Maofisa, wakaguzi na Askari
kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha usalama unaendelea kuimarika mkoani
hapa hasa katika kuzuia vitendo vya uhalifu.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna
Msaidizi Mwandamizi (SACP). Theopista Mallya amemshukuru DCP. Mushy na kuahidi
kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuongeza imani yao kwa jeshi la
Polisi.
Ukaguzi huo ni rasmi kwa mujibu wa Amri za kudumu
za Jeshi la Polisi Tanzania.
Gwaride maalumu la Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe likiwa katika mapokezi ya Mkuu wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma mara baada ya kuwasili mkoani humo.
Mkuu wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma, akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP). Theopista Mallya (kulia)
Mkuu wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma, akizungumza na viongozi wa jeshi la polisi mkoani humo.
Maafisa wa Polisi wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe wakimsubiri Mkuu wa Interpol Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Gemini Sebastian Mushy kutoka Kamisheni ya Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma kwa ajili ya kikao maalumu wakati wa ziara hiyo.
0 Comments