MKUU WA MKOA DODOMA AIPONGEZA MSD KWA MABORESHO YA UTENDAJI KAZI

Subscribe Us

MKUU WA MKOA DODOMA AIPONGEZA MSD KWA MABORESHO YA UTENDAJI KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai, akizungumza na wadau wa MSD katika mkutano mkuu wa mwake uliofanyika jijini Dodoma Aprili 6, 2024.

.................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameupongeza uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kwa mabadiliko makubwa yanayoendelea katika taasisi hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa yamewezesha kupunguza malalamiko ya uhaba wa bidhaa za afya nchini, mathalani malalamiko ya uhaba wa dawa.

Senyamule ameeleza kwamba awali wakienda kwenye mikutano ya hadhara kuongea na wananchi, walikumbana na malalamiko mengi ya uhaba wa dawa, lakini hivi karibuni hali imebadilika, japokuwa bado kuna changamoto, lakini angalau inatia moyo kuona kuna mageuzi yanafanyika. 

Senyamule ametoa pongezi hizo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wateja na wadau wa MSD Kanda ya Dodoma, ambao ni kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Halmashauri ya Kiteto, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OSHA jijini Dodoma.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kwamba huwezi kuongelea maendeleo ya sekta ya afya bila kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani ameleta mapinduzi makubwa, katika kipindi kifupi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

“Tunapoongelea maboresho ya sekta ya afya na mabadiliko ya huduma hatuwezi kuacha kumtaja Mhe. Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan, kama kiongozi mkuu aliyeongoza mapinduzi haya, kwani tumeshuhudia ongezeko kubwa la bajeti ya bidhaa za afya, miundombinu ya afya, ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya, ongezeko la vifaa tiba katika ngazi zote za kutolea huduma kuanzia ngazi ya chini mpaka taifa” Alisema Mhe. Senyamule

Aidha, Mhe. Senyamule ameipongeza MSD kwa kuratibu mikutano hiyo ya wadau, kwani vikao hivyo ni daraja muhimu katika kuboresha mahusiano na mawasiliano baina ya pande hizo, kuwapa uelewa wadau namna MSD inavyofanya kazi na mifumo iliyopo, kudumisha umoja na kuwahudumia wananchi kwa wakati, kupeana mrejesho wa huduma zinazotolewa, kuainisha changamoto zinazojitokeza kwenye mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya na kuhakikisha zinapatiwa majibu ili kuleta tija.

Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule ametoa rai kwa watendaji wa sekta ya afya kuvisimamia vyema vituo vya kutolea huduma ili waweze kukusanya mapato ya kutosha, kusimamia thabiti mnyororo wa ugavi wa bidhaa.@msdtanzania.Meneja wa MSD Kanda ya Kati Mwashehe Jumaa akitoa taarifa katika kikao hicho.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akikabidhi vyeti vya kutambua mchango wa wadau wa MSD. 

Vyeti kwa wadau wa MSD vikitolewa.
Wadau wa MSD wa Kanda ya Kati wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wa MSD kutoka Dodoma na Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
 

Post a Comment

0 Comments