Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania
(TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeandaa kongamano la vijana kuhusu rushwa na dawa
za kulevya.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Sipha
Mwanjala akizungumza na waandishi wa habari Aprili 5, 2024 alisema kuwa
kongamano hilo limewahusisha vijana zaidi ili wajue madhara ya rushwa na
matumizi ya dawa za kulevya.
"Kongamano hili ni la muhimu sana kwa kundi
la vijana na makundi mengine na ndio maana sisi kama TAKUKURU tulifanye ili
jamii iweze kujua madhara ya rushwa na matumizi ya dawa za kulevya,"
alisema Mwanjala.
Alisema mada moja ya mada itakayotolewa ni wajibu
wa vijana katika kuzuia na kupambana na rushwa na kuwa washiriki wa kongamano
hilo ni Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Chuo cha Maji,
Chuo cha Afya na Chuo cha Utumishi vyote vya Singida.
Mwanjala ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali kushiriki kongamano hilo ambalo ni muhimu sana ambalo litafanyika kesho Aprili 6, 2024 ukumbi wa Uhasibu kuanzia saa 4: 00 asubuhi.
0 Comments