Bidhaa za Afya zikipakiwa kwenye gari jingine kutoka kwenye lori la Bohari ya Dawa (MSD) baada ya kufikishwa Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuvigawa kwa waathirika wa mafuriko leo Aprili 8, 2024.
.......................................
MSD YAKABIDHI BIDHAA ZA AFYA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI
Na Mwandishi Wetu, Rufiji, Pwani
BOHARI ya Dawa (MSD) leo Aprili 8, 2024
imekabidhi bidhaa za afya mbalimbali kwa waathrika wa mafuriko Wilayani Rufiji
mkoani Pwani.
Bidhaa hizo zimekabidhiwa kituo cha Afya Mohoro kilichopo Halmashauri
ya Wilaya ya Rufiji ambazo ni pamoja na
Dawa, za kuzuia na kutibu malaria,
kuhara na yale ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Kwa upnde wa vifaa tiba ni pamoja na magodoro, mashuka na vyandarua, milingoti ya
kutundikia maji tiba ( Drip Stand), Binliners na vifaa vingine vitakavyosaidia
katika zoezi hili.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bidhaa hizo
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dr. Hamis Abdallah. ameishukuru MSD kwa
juhudi za haraka zilizofanyika kuweza
kuwafikia wahanga wa mafuriko. Ameongeza kuwa bidhaa hizo zitasaidia katika
utoaji wa huduma kwa waathirika wa mafuriko.
Naye meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Betia Kaema amesema MSD baada ya kuona taarifa ya janga hili iliamua kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwasiliana na mamlaka za Wilaya ili kufahamu mahitaji yanayotakiwa kwa waathirika. “Leo tumekabidhi vifaa ili kuhakikisha huduma za afya hazisimami kwa wananchi, lakini pia tumetembelea maeneo mbalimbali kujionea hathari za mafuriko haya.MSD itaendelea kutoa ushirikiano mpaka pale hali itakapotengamaa." alisema Betia.
0 Comments