MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TABORA : WAZAZI WAPATIENI WATOTO WENU ELIMU YA MAADILI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Uyui mkoani Tabora Shaffin Ahmedal Suma (Aliyevaa kofia) akikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa viongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui ikiwa ni moja ya tukio la kuadhimisha siku ya jumuiya hiyo.
...........................
Na Nyamizi Moses (Singidani Blog) Tabora.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wilayani Uyui mkoani
Tabora Shaffin Ahmedal Suma amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto
wanapata elimu ya kutosha na kuwalea katika maadili mema yanayopendeza katika
jamii.
Shaffin Suma ameyasema hayo wakati wa maadhimisho
ya siku ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilayani humo na kuwataka wazazi kuwa mstari
wa mbele katika kufundisha vijana wao maadili mema na kupata elimu ya
kutosha.
"Niwaombeni ndugu zangu wazazi na walezi tuhakikishe vijana wetu
huko majumbani wanapata elimu inayostahili,lakini pia tuhakikishe hawa vijana
wetu tunawapatia maadili mema yatakayofanya jamii ijivunie kijana wako"
alisema Suma.
Suma ameongeza na kusema kuwa ni wa jibu wa Kila
mzazi kusimamia makuzi bora ya mtoto wake haswa katika masomo pamoja na
kuendeleza lugha adhimu ya kiswahili.
"Ni vyema sana kwa sisi wazazi kuwa fatilia watoto wetu hatua kwa
hatua ili tuhakikishe kuwa wanafanya mambo mema katika jamii, lakini kumekuwa
nwa tabia ya baadhi ya watoto wetu wanaleta tabia za nje na kuacha kuitukuza
lugha yetu adhimu ya kiswahili niwaombe wazazi tu jitahidi kuwafundisha watoto
utamaduni wetu pia Kuna fursa itakuja kwa watoto wetu kwenda nje kuwafundisha
kiswahili lakini pasipo kujua wataendaje? kwa hiyo tulisimamie hili".
alisema Suma.
Aidha ametoa zawadi kwa wa mama waliojifungua
katika hospital hio ikiwa ni moja wapo ya kuunga Mkono juhudi za Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu hassan katika kuboresha huduma
ya Mama na mtoto.
"jumuiya ya wazazi imeona ni vyema kutoa
zawadi hizi kidogo kwa wa mama hawa waliojifungua katika hospitali hii kwahiyo
kwa hiki kidogo alichotujaalia Mungu tumeona tuwape wa mama hawa" alisema
Suma .
Pia Suma ametoa kiasi cha shilingi milioni moja
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwa shule ya ikonola iliyopo katika kata ya isikizya
wilayani Uyui.
"Elimu ni muhimu na mimi ni muumini wa Maendeleo ya elimu katika
jamii,mimi kama Mwenyekiti wa wilaya niko tayari na nitachangia Kiasi cha
shilingi milioni moja ili watoto wetu wajifunze vyema na walimu waishi
vyema". alisema Suma,
Maadhimisho hayo yameambatana na upandaji miti pamoja na kutoa vifaa Vya usafi vyenye thamani ya Sh. 400,000 katika Hospital ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Uyui mkoani Tabora Shaffin Ahmedal Suma, akiwasalimia wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Uyui.
No comments