Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akiwa kwenye swala ya Eid El-Fitri iliyofanyika Msikiti wa TAQWA.
Swala ikiendelea.
Swala ya Eid El-Fitri ikiendelea
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye swala ya Eid El-Fitri
Swala ikiendelea.
Waumini wa dini hiyo wakiswali nje ya Msikiti wa TAQWA
Picha za pamoja baada ya swala hiyo..
Na Dotto Mwaibale-SINGIDANI BLOG
SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro
amesema madiwani wa Manispaa ya Singida wanaoruhusu kupitisha vibali vya kuuza
nyama ya nguruwe 'Kitimoto' kwenye maeneo ya makazi ya watu Waislamu mkoani
hapa hawata wapigia kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika 2025.
Akizungumza kwenye swala ya Eid El-Fitri iliyofanyika katika Msikiti wa Taqwa mjini hapa. Sheikh Nassoro alisema jambo hilo la kuzagaa kwa vijiwe vya kitimoto kila kona mjini hapa linachangiwa kwa kiasi kikubwa na madiwani wanapokuwa kwenye vikao vyao na kuruhusu leseni ya kufanya biashara hiyo.
" Biashara ya kuuza nyama choma ya nguruwe inatakiwa ifanyike kwenye maeneo maalumu tena huko nje ya mji lakini siku hizi kila kona hapa mjini kuna vijiwe vya kitimoto vingine vipo mbele ya nyumba za watu na misikiti ya kufanyia ibada jambo ili halikubaliki hata kidogo madiwani waislamu ambao maeneo yao yana vijiwe hivyo vya kitimoto hatuta wapigia kura," alisema Sheikh Nassoro.
---ANGALIA VIDEO---
0 Comments