Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (katikati) akiwaelekeza jambo vijana wa Skauti wakati alipokuwa akiwahimiza kujikita katika kilimo na ufugaji alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mkoa wa Singida kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana hao.
................................
Na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
AFISA Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka Vijana Mkoani
Singida waliopo katika Vyuo, Shule za
Misingi na Sekondari kuanzisha miradi ya kilimo (Bustani) pamoja na ufugaji
katika maeneo ya shule na vyuo wanavyosoma.
Ndahani ameyasema hayo wakati wa ziara ya
kugakagua miradi ya Vijana wa Skauti katika vyuo, shule za msingi na sekondari
alipoifanya katika Chuo cha Maendeleo (FDC) Singida.
Ndahani amesema ni wajibu wa uongozi wa vyuo na
shule kutenga maeneo maluumu watakayo tumia vijana katika kujifunza na
kuendeleza kilimo na ufugaji kwenye maeneo ya shule na kuwa shule nyingi
za Mkoa wa Singida zina maeneo ya
kutosha lakini hayatumika katika uzalishaji au mafunzo ya kilimo au mifugo
ambayo inasababisha watu kuyavamia na kuanzisha migogoro baina ya shule na
wananchi.
"Kwa kufanya hivi tutakuwa tumesaidia vijana
wetu kupata uzoefu na kupenda kulima na kufuga badala ya kukichukia
kilimo," alisema Ndahani.
Alisema katika nchi yetu ipo fursa kubwa katika
sekta ya kilimo na ufugaji na Serikali imeweka mazingira mazuri ya vijana
katika kilimo ambapo Serikali hutoa mbolea ya ruzuku nchi nzima pamoja na mbegu
ya alizeti ambayo ndiyo zao kuu la biashara katika mkoa wetu.
Kijana Suphiani Nurduni ambaye ni kiongozi wa
kundi la Skauti Tawi la Chuo cha FDC amesema wameamua kujikita katika kilimo
cha mboga kwasababu kuna fursa kubwa ya kibiashara kwa kuwa kila familia na wanachuo huhitaji
mboga kwa ajili ya chakula.
Mkufunzi wa chuo hicho, Samwel Tarimo ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za kilimo na ufugaji chuoni amemshukuru Ndahani kwa kufanya ziara na kutembelea shughuli za kilimo na mifugo inayotekelezwa katika Chuo cha FDC.Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (katikati(katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana hao.Muonekano wa bustani inayosimamiwa na vijana hao wa chuoo hicho cha Maendeleo.
Muonekano wa mazao katika bustani hiyo.
0 Comments