DC URAMBO KUTAFUTA MUAROBAINI UHUJUMU ZAO LA PAMBA
Mkuu wa Wilaya ya Urambo ambaye pia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Elibariki Bajuta akizungumza na wananchi pamoja na Wataalamu wa Wilaya ya Urambo kuhusu zao la Tumbaku katika kikao kilichofanyika Aprili 30, 2024.
.............................
Na Nyamizi Moses, Singidani Blog, Tabora
MKUU wa Wilaya ya Urambo ambaye pia ni Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Elibariki Bajuta amesema kumekuwa na hujuma
mkubwa katika zao la tumbaku.
Kamishna Bajuta ameyasema hayo wilayani Urambo wakati
akizungumza na Madiwani,Wataalamu wa
Halmashauri ya wilaya, Vyama vya Msingi, Watendaji Kata na Vijiji,
Wenyeviti wa Vijiji na kusema kuwa kumekuwa na uhujumu mkubwa wa zao la tumbaku
hali inayosababisha kuwepo kwa migogoro ndani ya vyama vya msingi.
Aidha, Bajuta amesema madhara yatokanayo na
utoroshwaji wa Tumbaku ni Halmashauri kukosa mapato, mikopo ya banki
kutorejeshwa, Vyama vya msingi kushindwa kufanya majukumu yake na wananchi
kuendelea kuwa maskini.
Hata hivyo Bajuta amesema itaundwa tume maalumu ya kufatilia na kudhibiti uhujumu wa tumbaku wilayani humo.
No comments