" />

HABARI ZA HIVI PUNDE

SERIKALI YARIDHIA KUTOA FEDHA ZOTE KUMALIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA USAGARI

Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Uyui, Almas Maige

.................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imeridhia kutoa fedha zote za kujenga Kituo cha Afya cha Kijiji cha Migungumalo Kata ya Usagari Wilaya ya Uyui. Mkoani Tabora. Leo nina habari nzuri kwa jimbo la Tabora Kaskazini Uyui.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Uyui, Almas Maige wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma mbapo pia Wizara ya Maji nayo imeridhia maombi ya Mbunge ya kuchimba visima sehemu ambako hakuna bomba la Ziwa Viktoria.

Maige ameyataja maeneo hayo kuwa ni Sitage Kijiji cha Mbeya Kata ya Igulungu, Kijiji cha Katunda Kata ya Mabama, Kijiji cha Azimio Kata ya Usagari na Kijiji cha Ndoba Kata ya Makazi.

Serikali pia Imeridhia maombi ya mbunge huyo ya kupanua Bomba la maji ya Ziwa Viktoria kwenda vijiji vya Nsimbo, Kagera, Huyari ya Moyo na Mputi.

“ Kwa niaba ya wana Uyui Kaskazini namshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha upendo na kuwajali wananchi wa Uyui,” alisema Maige.


No comments