Mkuu wa Wilaya ya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero katika Kata ya Msowero ambapo wananchi waliibua sakata la kuuzwa kwa mlima wa kijiji.
........................
Na Mwandishi Wetu, Kilosa
JESHI la Polisi wilayani Kilosa mkoani Morogoro limewatia mbaroni watu
wawili akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msowero A, Petro Sanga (Paroko)
mwenzake, Awadh Ngajime kwa tuhuma za kuuza eneo la mlima, mali ya kijiji cha
Msowero wilayani Kilosa.
Pia, inaendelea kuwatafuta watu wengine 48 ambao wanaosadikiwa kuwa sehemu
ya mtandao uliohusika kuuza kinyume na utaratibu jumla ya ekari 1158 za Kijiji
zilizopo katika mlima huo.
Hayo yalibainika wakati wa mkutano
wa hadhara kusikiliza kero za wanachi katika Kata ya Msowero uliotishwa na Mkuu
wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka mwishoni mwa wiki kijjijini hapo.
Shaka alisema kumekuwa na wimbi la uvamizi wa maeneo ya ardhi unaoonekana
kukithiri siku hadi siku na baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa wakihusika kuyauza
kinyume na sheria.
"Tuna kata saba ndani ya wilaya hii zinaongoza kwa migogoro ya ardhi
ikiwemo hii ya Msowero, mnaongoza mnavamia maeneo ya serikali, viongozi wapo
mnashirikiana nao wengine kisha mnageuka mnasingizia viongozi wa wilaya mkoa na
taifa kuwa wanakuja kupora ardhi yenu kumbe ni uongo kabisa.
"Mmeuza mlima kinyume na utaratibu ekari 1,158 zote mmevamia na kuuza
hii ni mali ya serikali ya kijiji kisha mnageuka kushutumu wengine kumbe
ninyi wenyewe ndio wahusika, Ocd Huyu
mwenyekiti aliyeshiriki kuratibu mauziano na kulipwa 500,000 na huyu aliuza
eneo la mlima kwa sh 20,000,000 naondoka nao, pia naagiza watu wengine 48
waliohusika kwenye kuuza wajisalimishe polisi,
vinginevyo watafutwe popote walipo na wafikishwa kwenye vyombo vya
sheria," alisema.
Hata hivyo, Shaka alipiga marufuku na kuweka zuwio la kuendeleza shuhuli
yoyote katika eneo la mlima unaodaiwa kuuzwa huku akisisitiza kuwa walioziwa
maeneo hayo wametapeliwa na bado ni mali ya Serikali.
"Viongozi mpo mnayaona kitongoji, kijiji, kata wote mnajua lakini
mnalea uovu huu, haiwezekani kila aliyehusika kwenye hili hatabaki salama ili
iwe fundisho kwa wengine, naomba wajuilisheni wote walionunua eneo lile
wametapeliwa na hatutasita kuchukua hatua kwa yoyote atakaekaidi maelekezo ya
serikali.
"Kibaya zaidi baada kufanya uovu mnatafuta watetezi ambao na wao kwa
kukosa busara na sababu wanatafuta umarufu wa kisiasa, wanalibeba jambo bila kulifanyia utafiti na
kujridhisha kumbe mnawaingiza mkenge.
"Nilishangaa sana viongozi wa chama kimoja cha siasa wakilibeba jambo
hili wqkidai wananchi wananyanganywa ardhi wanapigwa na kuindoshwa katika
maeneo yao, kumbe mumewalisha matango pori mnaficha uovu wenu na wao kwa kwa
vile maarifa yao madogo wakaona ndio ajenda ya kuibeba limebuma sasa warudi kukanusha
uongo waliouaninisha umma wa watanzania. Alifafanua Shaka.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Msowero Abdalla Machera alimueleza mkuu wa wilaya
kuwa katika siku za karibuni viongpzi wa kisiasa wamekuwa wakifika katika
maeneo yao huku wakilazimisha wananchi kupigwa picha na kutoa malalamiko ama
shutuma za uongo dhidi ya serikali jambo
ambalo amesema sio la kiungwa na kistarabu.
" Mhe DC unayoyasikia huko ni kutaka kuchafua kata yetu na viongozi
wetu ninyi ili wao kutafuta kuungwa mkono kwa mambo ya uongo na uzushi, yaliopo
hapa ni baadhi ya wananchi kujihusisha katika matendo maovu sasa wakiona
mnataka kuwachukulia hatua wanakimbilia kwa viongozi wa kisiasa ili wapaze
sauti wakidhania wanaweza kuzima uovu wao wasichukuliwe hatua kwa makosa yao, haiwezekani, wameuza mlima wetu ekari
1158" Alisema Abdallah mKweche mkti
wa kijiji Msowero
Jumla ya wananchi 50 wanadaiwa kuhusika katika kuuza Mlima Gongwe wenye ukubwa wa ekari 1128 kwa watu mbali mbali kutoka nje ya wilaya kwa ajili ya shuhuli za kilimo na ujenzi wa makaazi na wengine kuvamia kuweka maakazi na kilomo ambapo imebainika kuna uharibifu mkubwa wa mazingira.














No comments:
Post a Comment