Na Dotto
Mwaibale, Singidani Blog
KANISA la
Moravian Tanzania Mission ya Singida iliyopo chini ya Jimbo la Magharibi Tabora
limeanzisha harambee kwa ajili ya kupata fedha zaidi ya Sh. Milioni 250 za
ujenga wa makao makuu ya jimbo hilo Kusini Kati Singida.
Akizungumza
kwenye ibada ya Pentekosti iliyofanyika sanjari na uzinduzi wa harambee hiyo
iliyoongozwa na Askofu wa kanaisa hilo Jimbo la Magharibi Tabora, Mchungaji
Ezekiel Yona na kuhudhuriwa na Wachungaji wanafunzi zaidi ya 40 kutoka Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha kanisa hilo kilichopo Mkoa wa Mbeya
kupitia umoja wao ujulikanao kama Umoja wa Wanafunzi wa Theologia (UWATHETE),
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi, Edward Mdaki alisema kiasi hicho cha fedha
ndicho kinachohitajika ili kuanza ujenzi huo.
Alisema eneo la Mission ya Singida lilianzishwa mwaka 2017 na mpaka sasa lina miaka saba na makao makuu yake yapo Singida mjini na lina jumla ya Parishi 39, Shirika 80 na waumini wasiopungua 27,000.
Alisema
makao makuu ya jimbo hilo yatajengwa katika viwanja vya kanisa hilo eneo la
Mandewa lililopo nyuma ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida.
Kiongozi wa
msafara wa wanafunzi hao kutoka Chuo Kikuu cha TEKU ambaye pia ni Mhadhiri wa
chuo hicho, Mchungaji Ezekiel Majani
alisema huduma ya kwenda maeneo mbalimbali ya nchi kuinjilisha waliianza miaka
mitano iliyopita ambapo mwaka juzi walikuwa Mtwara, mwaka jana Rukwa na mwaka
huu Mkoa wa Singida.
Mchungaji
Majani alitumia nafasi hiyo kumuomba Askofu Ezekiel Yona kuwaomba viongozi wa
kanisa hilo kuwasaidia kuwawezesha kupata fedha zitakazo wasaidia katika
shughuli mbalimbali za uinjilishaji ikiwa ni chakula, mafuta ya gari pamoja na
mahitaji mengine kwa ajili ya kufanya matendo ya huruma kwa wahitaji.
“Baba
Askofu tuna changamoto kubwa ya kupata fedha za huduma hii tumekuwa
tukichangishana sisi wenyewe wanafunzi jambo ambalo tunashindwa kuyafikia
malengo yetu tunakuomba ukatuombee kwa viongozi wenzako,” alisema Mchungaji
Majani.
Askofu Yona
akipokea maombi hayo alimtaka Mchungaji Majani kuandaa mpango wa huduma hiyo
ambao atauchukua na kuwapelekea viongozi wenzake ili kupata njia bora ya
kuwasaidia na kuwa jambo hilo linawezekana.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye changizo hilo,
Erick Simkwembe alisema Serikali inajua mchango mkuwa wa makanisa ambapo
alitumia nafasi hiyo kuyaomba kuendelea na mchango wao wa kuyalea makundi ya
vijana na wanawake katika makanisa yao.
“Baba
Askofu kanisa linanafasi kubwa kuhakikisha maadili katika nchi yetu yana baki
kuwa katika mstari sahihi kuna baadhi ya watu wanaweza kukemewa na kiongozi wa
Serikali kuhusu ukosefu wa maadili na akawa mkali kujirekebisha lakini mtu huyo
huyo akionywa na kiongozi wa dini anamsikiliza,” alisema Simkwembe.
Kwa upande
wake Mkuu wa Kitengo cha Polisi Ushirikishi Jamii Mkoa wa Singida, ACP Hamisi
Mungwana alilipongeza kanisa hilo kwa kuwa mstari wa mbele kwa mambo mbalimbali
kama vile kuanzisha chuo kikuu ambacho kinatumika kutoa elimu kwa makundi ya
watu mbalimbali huo ni mchango mkubwa kwa Serikali.
“Nilipongeze
kanisa kwa kufanya doria ya kiroho na sisi kama jeshi la Polisi huwa tunafanya
doria ya nadharia ya kutembea mitaani kuangalia usalama wa raia na mali zao
nafikiri huwa munatuona,” alisema ACP Mungwana.
Kiongozi wa msafara wa wanafunzi hao kutoka Chuo Kikuu cha TEKU ambaye pia ni Mhadhiri wa chuo hicho, Mchungaji Ezekiel Majani akizungumza kwenye ibada hiyo.
































No comments:
Post a Comment