MEI MOSI NI SIKU YA TAFAKURI KWA WATUMISHI-MAJALIWA
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambayo
huadhimishwa kila mwaka ni siku maalum kwa ajili ya wafanyakazi kutafakari na
kutathmini namna walivyotekeleza malengo waliyojiwekea katika mwaka husika.
Amesema kuwa siku hiyo inatoa fursa kwa
wafanyakazi wote duniani kuweka mipango kwa ajili ya mwaka unaofuata na ndiyo
maana inafanyika kipindi ambacho nchini nyingi duniani zinakuwa katika
maandalizi ya Bajeti.
Amesema hayo leo (Jumatano Mei Mosi,
2024) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani inayofanyika kitaifa
mkoani Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mgeni Rasmi katika
maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye
amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Siku hii ni muhimu sana na
inatukumbusha wajibu wetu wafanyakazi wa kujadiliana kwa pamoja changamoto
zilizopo katika utendaji wetu wa kazi na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja na
hatimaye kuleta tija katika maeneo ya kazi”.
Aidha,
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya
katika kuwaletea watanzania maendeleo. “Sisi sote ni mashahidi wa mafanikio
makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu kiuchumi, kisiasa,
kidiplomasia na kijamii”
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha
No comments