Mgombea Nafasi ya Ubunge , Haiderali Gulamali wa Jimbo la Ilongero lililopo Wilaya ya Singida mkoani Singida akihutubia wananchi na Wana CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu 2025 jimboni humo.
.................................................
Dotto Mwaibale na
Philemoni Solomon Singida
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kushika dola kwa
sababu ya umoja uliojengeka tangu nchi yetu ipate uhuru.
Hayo yamesemwa na Mgombea Nafasi ya Ubunge, Haiderali
Gulamali wa Jimbo la Ilongero lililopo
Wilaya ya Singida mkoani Singida wakati akihutubia wananchi na Wana CCM wakati
wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu 2025.
“ Tuliojitokeza kugombea nafasi ya ubunge tulikuwa wengi
lakini mnaona jinsi wenzangu ambao hawakubahatika kuchaguliwa walivyofika
kuniunga mkono na wengine wamevuka mpaka kwa kutoa fedha zao kuwachangia
madiwani,” alisema Gulamali.
Gulamali aliongeza
kuwa hicho ndiyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kila Mwana Ilongero na
watanzania wanajivunia uwepo wake.
Gulamali alisema kuwa chama hicho kinaendelea kushika dola
kutokana na demokrasia na uwazi ilionao ndani ya chama hicho kikubwa si kwa
Tanzania pekee bali na Afrika kwa ujumla.
Alisema amegombea nafasi hiyo siyo kwa ajili ya kupata fedha
bali kuwiwa kuwatumikia wana Ilongero na wananchi kwa ujumla.
Alitumia nafasi hiyo kukishukuru chama hicho kwa kumuamini
kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ambapo ameahidi kuwatumikia wananchi kadri
atakavyo jaaliwa na Mwenyezi Mungu.
Gulamali atakuwa
mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya la Ilongero zamani likiitwa Jimbo
la Singida Kaskazini.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Waziri mstaafu Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
akizungumza kwenye uzinduzi huo aliwataka kila mwananchi mwenye kadi ya kupigia
kura kujitokeza kwenda kupiga kura nyingi kwa wagombea wanaotokana na CCM
kuanzia za Rais, wabunge na madiwani.
“Tunahitaji Mkoa wa Singida uwe kinara wa
kura zote katika uchaguzi mkuu na hilo linawezekana kutokana na umoja wetu
tulionao”, alisema Nyalandu huku akishangiliwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata alisema demokrasia
iliyomo ndani ya chama hicho ndiyo inakifanya kionekane tofauti na vyama
vingine kutokana na kuwapata viongozi wake kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa
kwa kuchaguliwa.

Mgombea Nafasi ya Ubunge, Haiderali Gulamali wa Jimbo la Ilongero lililopo Wilaya ya Singida mkoani Singida akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye uzinduzi huo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Pamba cha Biosustain, Sajjad Haider akizungumza kwenye uzinduzi huo
Wagombea nafasi ya udiwani wa jimbo hilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mgombea Nafasi ya Ubunge, Haiderali Gulamali wa Jimbo la Ilongero akiteta jambo na mke wake wakati wa uzinduzi huo.
Mke wa Mgombea Nafasi ya Ubunge, Haiderali Gulamali wa Jimbo la Ilongero (kushoto) akiwa na mtoto wao.
Uzinduzi ukiendelea
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Shamrashamra zikiendelea wakati wa uzinduzi huo.
Watoto wa Gulamali wakiongoza shangwe kwenye uzinduzi huo.
Familia ya Gulamali ikifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo.
Familia ya Gulamali ikifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo.
Mgombea nafasi ya ubunge Jimbo la Ilongero akiwasili kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.
Mgombea nafasi ya ubunge jimbo la Ilongero akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.
Gari ya kampeni ikiongoza msafara kuelekea eneo la tukio.
Basi maalum la kampeni nchi nzima ambalo lipo chini ya Kada wa CCM Lazaro Nyalandu likiwa eneo la eneo ulipofanyika ufunguzi wa kampeni hizo.
Mgombea nafasi ya ubunge Jimbo la Ilongero akiwapungia mkono wananchi akiwa amepanda pikipiki (upande wa kushoto)
Kada wa CCM, Lazaro Nyalandu akisalimiana na wagombea nafasi za udiwani wa jimbo hilo.
Mgombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ilongero, Haiderali Gulamali (aliyesimama nyuma na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akiwa katika picha ya pamoja na wagombea nafasi ya udiwani wa jimbo hilo.
Mgombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ilongero, Haiderali Gulamali (aliyesimama nyuma na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akiwa katika picha ya pamoja na wagombea nafasi ya udiwani wa jimbo hilo.
0 Comments