POLISI SINGIDA YAWADAKA WATUHUMIWA 235 KWA MAKOSA MBALIMBALI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, May 7, 2024

POLISI SINGIDA YAWADAKA WATUHUMIWA 235 KWA MAKOSA MBALIMBALI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Amon Kakwale akitoa taarifa kwa waandishi wa habari. 

.......................................

Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog

JESHI Ia Polisi Mkoa wa Singida Iimeendelea kufanya kazi zake za kulinda raia na mali zao kwa kufanya doria na misako ili kubaini, kutanzua na kuzuia uharifu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 235.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Amon Kakwale akitoa taarifa kwa waandishi wa habari alisema katika kipindi cha Februari hadi Aprili, 2024 jeshi hilo lilifanya misako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 235 wa makosa mbalimbali ya jinai pamoja na baadhi ya vielelezo vinavyo waunganisha watuhumiwa na makosa yao.

Alisema katika idadi hiyo ya watuhumiwa walikamatwa watuhumiwa 135 wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi zenye uzito wa Kg. 17.2, watuhumiwa 46 wakiwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi zenye uzito wa Kg. 92 na watuhumiwa 5 wakiwa na dawa za kulevya aina ya Heroini zenye uzito wa gramu 0.82.

Kakwale alisema kuwa vile vile, walikamatwa watuhumiwa 11 wakiwa na pombe ya moshi lita 123. watuhumiwa 3 wakiwa na ndoo kubwa 31 za mafuta ya kupikia aina ya Safi mali ya Mohamed Enterprises Limited zenye ujazo wa lita 20 kila moja. Wengine ni watuhumiwa 5 waliokamatwa na televisheni flat screen 6, ambazo ni Hisense inchi 43 moja, Sumsung Inch 65 moja, Sumsung Inch 40 moja na tv zingine mbili zikiwa zimefutwa majina ambazo ni mali za wizi.

CACP Kakwale alisema pamoja na hayo, walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na hujuma katika miundombinu ya umeme ambapo katika misako hiyo walikamatwa watuhumiwa 3 wakiwa na transfoma 1 50KVA namba TX006524 aina ya TCO yenye thamani ya Tshs. 7,500,0001= na nyaya za shaba.

Pia alisema walikamatwa watuhumiwa 3 wakiwa na miundo mbinu ya umeme wa TANESCO (polymeric post insulators) vipande 63, ambavyo walivifunga kwenye viroba 8 tayari kwa kivisafirisha kwenda kuviuza mkoani Mwanza na mtuhumiwa mmoja ambaye alikamatwa na mita moja ya umeme wa TANESCO.

Aliwataja watuhumiwa wengine ni pamoja na watuhumiwa 2 ambao walikamatwa wakiwa na betri 7 za minara ya simu aina ya NORTH STAR zenye uwezo wa N- 170 mali ya Kampuni ya HELOIS TOWER TANZANIA, watuhumiwa 4 walikamatwa kwa kosa la kukutwa na jenereta aina ya PARKING PORTABLE Ienye uzito wa Tani moja mali ya Kampuni ya minara ya simu ya NOVEN.

Alisema mtuhumiwa 1 kwa kosa la wizi wa matairi matano ya gari yakiwa na rimu zake, watuhumiwa 11 kwa makosa ya wizi wa pikipiki na watuhumiwa wanne kwa wizi wa pikipiki za magurudumu matatu (bajaji)

Alisema baada ya ukamataji huo, baadhi ya kesi bado zipo chini ya upelelezi na zingine zimefikishwa mahakamani zikiendelea kusikilizwa na zipo zilizopata mafanikio kwa watuhumiwa kuhukumiwa vifungo mbalimbambali.

Kakwale alitaja baadhi ya mafanikio ya kesi zilizofikishwa mahakamani kwa kipindi hicho ni pamoja na Mustafa Hamisi (35), kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti na kubaka. Musa Masanilo (35), amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka na Baraka Yohana (23). amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kupitia kikosi cha usalama barabarani limefanya doria na misako na kufanikiwa kuwakamata madereva wawili kwa makosa ya kuendesha magari kwa mwendo kasi usioruhusiwa kisheria. Madereva hao ni Athumani Mustapha Kasenya (34), dereva wa gari aina ya Basi lenye namba T.454 DHP mali ya Kampuni ya Matunduru  na Julius Dionice (39), dereva wa gari Basi T.937 EFK malI ya Kampuni ya SATCO.

Alisema kutokana na makosa hayo, madereva hao walifungiwa lesenI zao za udereva kwa kipindi cha miezi mitatu kwa uendeshaji wa gari kwa mwendo wa hatari na usiofaa jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wengine wa barabara.

Kakwale kwa niaba ya jeshi hilo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao 235 na vielelezo vilevile linawaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini waharifu wakamatwe mapema kabla hawajaleta madhara kwa jamii pia Jeshi la Polisi linawaomba wananchi waliopotelewa na vitu vyao vilivyotajwa hapo juu, wafike kwenye vituo vya wakiwa na risiti halisi za manunuzi ya vitu hivyo ili waweze kutambua na kukabidhiwa mali zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Amon Kakwale akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa hiyo.SACP Kakwale akionesha dawa za kulevya aina ya mirungi zilizokamatwa.
Hapa akionesha dawa za kulevya aina ya bange zilizokamatwa.
SACP Kakwale akionesha miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iliyokamatwa ikiwa imebebwa katika bajaji.
Akionesha bajaji iliyokuwa imebeba miundombinu ya TANESCO.
Kamanda Kakwale  akionesha Jenereta aina ya Parking Portable Ienye uzito wa Tani moja mali ya Kampuni ya minara ya simu ya NOVEN likioneshwa baada ya kuibiwa.

 Tranfoma mali ya TANESCO lililoibwa likioneshwa. (PICHA ZOTE NA SOLOMON PHILIMON)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad