SENGEREMA KUZIONA SIMBA, YANGA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, May 24, 2024

SENGEREMA KUZIONA SIMBA, YANGA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ akizungumza  baada ya  Kamati ya Siasa kutemmbelea mradi wa uwanja wa Mnadani. 
 Picha zote na Baltazar Mashaka
Mchumi wa Halmashauri ya Sengerema, Wilbad Bandola,leo akitoa  taarifa ya mradi wa uwanja wa michezo Mnadani kwa Kamati ya Siasa  ya CCM Mkoa wa Mwanza..

NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Sengerema imepongezwa  kwa ubunifu wa ujenzi wa uwanja wa michezo wilayani humo kuwa utachochea ukuaji wa michezo na mapato ya halmashauri hiyo.

Pongezi hizo zilitolewa  na Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart ‘ kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa, baada ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wilayani Sengerema. 

“Kamati tunapongeza kwa mradi huu wa uwanja unaokidhi mahitaji ya wananchi  wa Sengerema na halmashuri mtakusanya mapato sahihi kupitia michezo, pia ukikamilika mengi yatafanyika ambapo timu kubwa za Simba, Yanga na Pamba zitakuja kucheza hapa,” alisema Smart.

Alisema uwanja wa michezo Mnadani lilikuwa hitaji la  wananchi muda mrefu ,hivyo serikali ya awamu ya sita na uongozi wa halmashauri  kuridhia ujenzi huo kwa mapato ya ndani.

Aliwahimiza wananchi kuchapa kazi n kueleza kuwa serikali itaendelea kuleta fedha za miradi ya  maendeleo wafaidi matunda ya kodi zao.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, alisema serikali ni kuona mradi huo ukikamilika utasaidia kuinua michezo n mapato ya  Sengerema.

 “Timu ya Pamba itaweka kambi hapa pia nitamleta Diamond kuufungua  rasmi, hivyo fanyeni hima  mradi ukishakamilika  nitaileta Pamba na Yanga hapa,Sengerema  mtapata mapato hapa  Mnadani,”alisema .

Awali Ofisa Uchumi na Mipango wa Halmashauri ya Sengerema, Wilbad Bandola alisema lengo la kujenga uwanja wa michezo Mnadani ni maelekezo ya ilani ya CCM, utasaidia kuibua na kukuza vipaji na kuendeleza michezo .

Mbali na kuinua sekta ya michezo pia, uwanja huo utasaidia kuongeza mapato ya halmashauri kwa viingilio vya milangoni na vibanda  vya bbiashara vitakavyojengwa kuzunguka uwanja.

“Fedha za gharama za ujenzi ni sh. milioni 361.2 za mapato ya ndani, mfuko wa jimbo, ufadhili wa mbunge na wadau wa maendeleo.Awamu ya kwanza ya ujenzi utahusisha  uzio na miundombinu  mbalimbali , ukikamilika utakuwa n uwezo wa kubeba watazamaji 15,000 hadi 20,000 kwa wakati mmoja,”alisema Bandola.  

Alisema miundombinu inayoendelea kujengwa ni uzio (ukuta), matundu 24 ya vyoo   hadi  sasa sh. milioni 220.5 zimepokelewa kati ya sh.milioni 361.2  na zilizokwisha kutumika kwa ujenzi huo ni sh.milioni 189

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad