Mwandishi
wetu, Johannesburg SA
Baada ya kuzindua kitabu
kinachohusu Utengamano wa Afrika;
Mgogoro wa Sahara nchini Tanzania na
baadae Kenya, Watanzania wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanikiwa kukifikisha kitabu chao nchini
Afrika Kusini.
Wanahistoria hao Dk Maximilian Chuhila na James Zotto
wamefanikiwa kukipeleka kitabu chao
nchini Afrika Kusini wakilenga
kitumike kufundishia elimu ya juu katika nchi za Afrika.
Awali, Dk Chuhila na Zotto walifanya
uzinduzi wa kitabu hicho kilicho chapishwa na APE Network Chuo Kikuu Katoliki
cha Ruaha (Rucu) mkoani Iringa na baadae wakakipeleka Chuo Kikuu cha Kennyata,
Nchini Kenya.
Jana Juni 11, 2024 wahadhiri hao
walifanikiwa kufikisha maudhui ya kitabu hicho katika Chuo Kikuu cha
Johannesburg huku wakipata nafasi ya kuzungumza na wanahistoria mbalimbali kutoka nchini humo
wakiwamo wanafunzi na wahadhiri.
Dk Chuhila ambaye ni Mwenyekiti wa
Chama cha Historia nchini amesema kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu vilivyo
onyesha kwa undani masuala ya utengamano wa Afrika hasa kuhusu mgogoro wa
Sahara.
Kabla ya kuandika, Wanahistoria hao
wawili walifanya utafiti nchini Morroco kisha kuja na kitabu wanacho amini kama
kikitumika vyuo vikuu kitaongeza uelewa kuhusu utnganao wa Afrika hasa, mgogoro
huo wa Sahara.
Awali, Zotto alisema utengamano wa
Afrika ni silaha laini inayoweza kumaliza mzozo wa Sahara uliodumu kwa zaidi ya
miongo miwili sasa.
Morroco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi
Polisario zimekuwa zikilumbana kwa zaidi
ya miongo miwili kuhusiana na udhibiti
wa eneo hilo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa,
Jimson Sanga amesema jitihada za wanahistoria hao zinapaswa kuigwa na wahadhiri
wengine kwamba, badala ya kuandaa maudhui yanayoishia ndani ya nchi, wanaweza
kusambaza duniani kote.
“Binafsi nimeona kumbe inawezekana,
kama tunaweza kufanya tafiti za ndani ya nchi basi tunaweza kufanya tafiti nche
na maandiko yetu yakatumika katika kutoa elimu vyuo vikuu mbalimbali,” amesema
Sanga.
Amesema badala ya kuwa wanapokea
maandiko na vitabu kutoka mataifa mengine, wanaweza pia kusambaza maudhuo hayo
nje ya nchi.









No comments:
Post a Comment