WILAYA YA MKALAMA YAIBUKA KIDEDEA KWA HOJA CHACHE ZA CAG-RAIS SAMIA ATAJWA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, June 29, 2024

WILAYA YA MKALAMA YAIBUKA KIDEDEA KWA HOJA CHACHE ZA CAG-RAIS SAMIA ATAJWA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego (katikati( akizungumza kwenye kikao Maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za CAG kilichofanyika jana Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, James Mkwega.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega, akisitiza jambo kwenye kikao hicho.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos akisoma hoja za CAG katika kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, James Mkwega na kulia ni Makamu Mwenyekiti Mchungaji Emmanuel Kabea.

.............................


Na Dotto Mwaibale, Mkalama

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imeibuka kidedea kwa kuwa na hoja 14 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na kuzishinda halmashauri zingine sita za mkoa huo.

Hoja hizo katika kila wilaya ni kama ifuatavyo, Wilaya ya Itigi ilikuwa na hoja 45 na sasa zimebaki 15, Wilaya ya Ikungi hoja 28 na zilizobaki ni 17, Iramba hoja 75 ambazo zimebaki ni 22, Manyoni hoja 59,na  ambazo zimebaki kwa hatua mbalimbali za utekelezaji ni 17, Singida Manispaa zilikuwa hoja 64 na Wilaya ya Singida zilikuwa 54 na zilizobaki ni 16.

Kufuaatia ushindi huo mnono Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Asia Mesos, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo James Mkwega pamoja na timu yao ya wataalamu wamepongezwa kwa nyakati tofauti wakati wa kikao maalumu cha Baraza la madiwani kilichoketi jana kwa ajili ya kupitia hoja za CAG. 

 Akizungumza Juni 28, 2024 katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego alitoa miezi mitatu kwa halmashauri hizo kuhakikisha ndani ya kipindi hicho ziwe zimezimaliza hoja zote ambazo zinatia dosari.

“Leo nipo halmashauri ya sita na sisi kama mkoa tunasubiriana hadi Septemba 30, 2024 hoja zote ziwe zimemalizika kuendelea kuwa nazo ni kuyakumbatia mapungufu yale aliyoyaona CAG,” alisema  Dendego.

Dendego aliziomba halmashauri hizo kupitia kamati zao za fedha zifanye kila linalowezekana kuhakikisha ndani ya miezi hiyo hoja zote ziwe zimefungwa ambapo pia alitoa angalizo kwa wakuu wa idara kuwa mtu yeyeyote atakayebainika kuzaliza hoja atawajibika mwenyewe kuzijibu kwani yeye na viongozi wengine hawataitisha kikao kuzijibu.

“Kutengeneza hoja binafsi nachukulia kama kula bila kunawa, sitegemei katika ustaarabu huo tulionao wa 2024 kwamba kunawatanzania bado wanakula bila ya kunawa,” alisisitiza Dendego.

Dendego aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kutokuwa sehemu ya watu ambao wanalalamika kutokukamilika kwa miradi badala yake wachukue hatua kama sheria inavyoelekeza ya kumshughulikia mtu yeyeyote ambaye watamuona anataka kuwarudisha nyuma.

Aidha Dendego alisema Rais Samia, Mama wa Taifa na Chifu Hangaya amekuwa akitoa fedha nyingi za kutekeleza miradi katika mikoa yote lakini atashangaa kuona mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi yetu kama Katavi na mingine ikikamilisha miradi yao kwa wakati na Mkoa wa Singida ukishindwa kwa madai eti fedha hazitoshi. Jambo hilo na mazoea ya namna hiyo kwake hayana nafasi.

“Singida mnamchanga wa kutosha, maji, mawe na viwanda tena mpo jirani na Mkoa wa Dodoma eti mnasema miradi inashindwa kukamilika kwa sababu hela hazitoshi acheni tabia hiyo mimi nataka kuona miradi inakamilika na chenji inabaki,” alisema Dendego.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida aliwataka wataalamu na maofisa watendaji mkoani humo kuwa wabunifu wa kutengeneza programu mbalimbali za kuinua uchumi na kuachakulalamikia na kuungana na makundi mengine ambayo yanamtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao.

“Ninyi wataalamu mnapaswa kuwa wabunifu tumieni elimu yenu kwa kuibua mipango yenye tija ambayo itaibua mambo mbalimbali ya kufanya na kutengeneza ajira kwenye maeneo yenu bada la ya kumtukana Rais ambaye anawapa mshahara jitokezeni bila ya kuona aibu kuyasema mambo yote ya maendeleo anayofanya Rais wetu,” alisisitiza Dendego.

Alisema katika suala la kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi yupo tayari kufanya kazi usiku na mchana na hata kulala ndani ya gari lakini ahakikishe kazi zinafanyika pasipo kukwama.

Katika hatua nyingine Dendegu alizitaka halmashauri za wilaya nazo zifanye utaratibu wa kukopa fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajiri ya kuwakopesha wananchi ili wazitumie kuanzisha miradi kama ya uchimbaji wa madini na kazi zingine ikiwa ni moja ya njia ya kuongeza kipato katika halmshauri hizo badala ya kuitegemea Serikali pekee.

“Nikija kwenye maeneo yenu ya kazi sitaki kusomewa taarifa kwenye karatasi nataka itoke katika kiganja chako cha mkono Rais akija hapa akiuliza nina watu wangapi mkoani hapa mnataka nimjibu kuwa sijui, mifugo mingapi sijui , kila nitakacho ulizwa nijibu sijui nitakuwa mkuu wa mkoa wa namna gani, mimi naweza nataka na nyinyi muweze na mtume salamu kwa wengine waambieni moto umewaka,” alisema Dendego.

Kwa heshima kubwa aliyompa Rais Samia Suluhu Hassan kuna watanzania zaidi ya milioni 60 kati ya hao 26 wameteuliwa kuwa wakuu wa mikoa nayeye akiwepo hivyo hawezi kulala usingizi atafanya kazi katika mazingira yoyole yale hata kulala ndani ya gari ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi na ubora.

Dendego kwake suala la elimu alisema ni la kufa na kupona atalisimamia na kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani wakiachwa mitaani ndio hao wanaoenda kuishambulia serikali mitandaaoni.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akichangia kuhusu ukamalishaji wa miradi kwa wakati alitoa ushauri kwa halmashauri hizo kuwatumia mafundi na wahandisi waliopo maeneo inapotekelezwa miradi hiyo kwa kuwapa mikataba ya muda mfupi ili utaalamu wao utumike kuongeza kasi ya kazi huku akiwataka wakurugenzi na watu wa idara ya manunuzi kuzunguka madukani kuona bei za vifaa vinavyouzwa na vile vifaa vitakavyouzwa kwa bei ya chini vinunuliwe badala kuachia mwanya wa kununua vifaa hivyo kwa bei ya juu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega  naye aliungana na viongozi wengine ambao wametaka ufungwaji wa hoja zote za CAG ndani ya muda uliopangwa ambapo alitumia kikao hicho kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali wilayani humo ukiwepo wa Kituo cha Afya cha Kata ya Gumanga.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali alisema wana Mkalama wasibweteke kwa ushindi huo waliopata wa kuwa na hoja chache za CAG kuliko halmashauri zingine ambapo aliwataka kuzipunguza hoja hizo ikiwezekana ziishe kabisa kwani huenda kuna halmashauri zingine hazi hoja hizo kabisa.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkalama, Agness Chuwa akitoa salamu za chama katika kikao hicho cha baraza la madiwani naye aliungana na viongozi wengine kuhakikisha hoja zote za CAG zinafungwa kwa wakati uliopangwa na wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ifanyike kwa thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Mkaguzi Mkuu Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Singida, Othman Jumbe aliwaeleza madiwani hao kuwa miradi hiyo inapokamilishwa ikamilishwe si kwa kuangalia majengo yalivyo bali majengo hayo yawe na ubora na thamani ya fedha zilizotolewa.

Akizungumzia ukamilishaji wa miradi hiyo yenye hoja alisema ni jukumu la halmashauri husika ya kuona namna ya kutafuta hela za kuimalizia na vingine miradi hiyo itaingizwa kwenye hoja ya mwaka mwingine wa fedha jambo ambalo sio zuri.

Katika baraza hilo madiwani walipata fursa ya kuchangia hoja mbalimbali huku hoja iliyohusu matengezo ya magari ambayo yamechukua muda mrefu tangu yaharibike yakiwa kwenye gereji mbalimbali ikichukua nafasi kubwa kujadiliwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega, akiongoza kikao hicho.
Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akichangia jambo kwenye kikao hicho. 
Mkaguzi Mkuu Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Singida, Othman Jumbe, akizungumzia ukamilishaji wa miradi katika halmashauri. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Shabani Mongomongo na Mkaguzi kutoka ofisi ya GAC, Mkoa wa Singida, Zainab Julius.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama, Peter Masindi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkalama, akielezea kesi nyingi zinazowahusu wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto wao shuleni (watoro) zinavyoshindwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Diwani wa Kata ya Miganga, Omari Mpinga Nzia akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalum, Zainabu Kihara kutoka Kata ya Kinyagiri kulia na Diwani mwenzake 
Wankembeta Timotheo kutoka Kata ya Ibaga wakiwa kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mkalama , Agness Chuwa akitoa salamu za chama kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Asia Mesos na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mchungaji Emmanuel Kabea.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Diwani viti maalumu, Florence Misai, Diwani wa viti maalumu, Habiba Omari na Diwani wa Kata ya Nduguti, Nduguti, Anthony Kahema.
Kikao hicho kikiendelea.

Diwani wa Kata ya Ilunda, Mohamed Imbele akichangia wakati wa kujibu hoja.

Diwani wa Kata ya Mwanga, Mohamed Juma akizungumza. 
Diwani wa Viti Maalumu, Mariam Kahola akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani viti maalumu, Florence Misai akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Nduguti, Anthony Kahema akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Kinampundu, Habiba Omari akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho cha baraza la madiwani maalumu la hoja za CAG.
Wakuu wa Idara, Viengo na Wataalamu wakiwa kwenye kikao hicho.


 Taswira ya kikao hicho wakati wa kujadili hoja za CAG.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad