Askari Polisi wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wakianya usafi wa mazingira katika baadhi ya mitaa ikiwa ni kuadhimisha siku ya utumishi wa umma.
...............................
Na Mwandishi Wetu, Manyoni.
ASKARI Polisi wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wamefanya usafi wa
mazingira katika baadhi ya mitaa ikiwa ni kuadhimisha siku ya utumishi wa umma
na kuunga mkono agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutunza mazingira.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Manyoni SP. Bakari Mzungu akizungumza na askari
hao alisema kazi ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo
itakuwa ni endelevu na lengo likiwa ni kuuweka mji wa Manyoni katika hali ya
usafi wakati wote.
“Napenda kuwaambia na kuwakumbusha kuwa usafi ni ustarabu ambao unalinda
afya zetu pamoja na mazingira tunayoishi hivyo ni wajibu wetu kujikita katika
kutunza na kuyaweka katika hali ya usafi maeneo yetu yote yanayotuzunguka jambo
litakalosaidia kutuepusha na magonjwa ya mlipo yanayosababishwa na uchafu,”
alisema Mzungu.
Mzungu aliwataka askari hao na wana Manyoni kufanya usafi katika maeneo yao
ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu Wilaya hiyo Kemirembe Lwota la kufanya usafi
kila Jumatano ya wiki na Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Mzungu alisema Polisi wanafanya usafi huo wa mazingira kwa madhumuni
makubwa mawili kuadhimisha siku ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi hiyo na
wanannchi ili wawaone polisi kama watu wa kawaida jambo litakaloimarisha
ushirikiano na kusaidia kuondoa uhalifu kwa kupata taarifa kutoka kwao kwa kuwa
wanaofanya uhalifu huo ni watu wanaoishi nao katika jamii.
Aidha, Mzungu alitaja jambo la pili kuwa ni kuimarisha uhusiano baina yao
na wananchi ambao wanawahudumia.
Usafi wa kuondoa uchafu kwenye mifereji ya kupitisha maji ukifanyika na askari hao.









No comments:
Post a Comment