Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi huo.Mashaka Kibaya,Tanga
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Mei 31, 2024, amezindua mradi wa
Airtel SmartWasomi utakaoendeshwa kwa kipindi cha miaka mitano huku Sh.128,262,608,000 zikitarajiwa kutumika ambazo ni sawa na dola za Marekani
USD 50,299,062.
Katika mradi uliozinduliwa, Kampuni ya Airtel Tanzania wanashirikiana na
Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, na kwenye utekelezaji
wake utaunganisha shule za Sekondari 3,000 na mtandao wa Airtel 4G kuwez00esha
upatikanaji bure wa maudhui ya kujifunza Kidijitali kutoka Maktaba mtandao ya
Mamlaka ya elimu Tanzania (TET).
Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba,kujifunza kidijitali ndio njia ya
haraka zaidi ya kuboresha matokeo ya kujifunza na kuandaa vijana huku
akibainisha kwa sasa uwiano wa Vitabu kwa mwanafunzi katika shule nyingi
haukidhi viwango vilivyowekwa na Serikali.
Majaliwa ameipongeza Airtel Tanzania na UNICEF kwa kuendeleza mpango huo wa
Airtel SmartWasomi unaosaidia juhudi za Serikali kwa lengo la kuongeza
upatikanaji wa elimu kwa vijana nchini.
Katika hotuba yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh
alisema, kwenye utekelezaji mradi utaunganisha shule za Sekondari 3,000 na
mtandao wa 4G kuwezesha upatikanaji bure wa maudhui ya kujifunza Kidijitali
kutoka Maktaba mtandao ya Mamlaka ya elimu Tanzania (TET).
Balsingh alisema kwamba, mpango wa Airtel SmartWasomi umekuwa na mafanikio
katika awamu ya majaribio na tayari imeunganisha shule 50 za Sekondari zilizopo
Zanzibar,Dodoma na Mbeya.
Alisema kuwa, mafunzo yametolewa kwa walimu zaidi ya 2,000 na hivyo
kuwafikia wanafunzi zaidi ya 55,000 wanaofundishwa na walimu hao na kwamba
mradi umefanya upembuzi wa kujua hali ya upatikanaji mtandao wa Intaneti ya
Airtel 4G kwa shule 4,200 na 500 huko Zanzibar.
Aidha Balsingh alisema kuwa, Airtel imeondoa malipo ya bando ili
kuwawezesha wanafunzi na walimu kusoma bure bila malipo ya Intanet kwenye
Maktaba ya mtandao ya taasisi ya elimu Tanzania na shule.
Kwa mujibu wa Balsingh, Airtel Tanzania ilianza utekelezaji dhamira yake ya
kusaidia elimu Kidijitali 2015 kwa kuzindua mradi wa VSOMO ikishirikiana na
mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi Veta.
Alibainisha kuwa utaratibu huo umekuwa ukifanyika kupitia aplikesheni
iliyopo kwenye Simu janja inayowezesha upatikanaji w kozi ya Veta bila kuwa na
haja kuhudhuria darasani.
Pia ameieleza Airtel kwamba, imekuwa na ushirikiano na DTB kwa kuzindua
maabara ya Kidijitali inayowajenga vijana na Wajasiriamali uwezo wa Tehama ili
kuweza kusimamia biashara zao kifanisi.
Naye Adolph Mkenda, Waziri wa elimu, Sayansi na teknolojia alisema, licha
ya Airtel SmartWasomi kupunguza mgawanyiko Kidijitali itaongeza tija kwa
wanafunzi kuendelea kujifunza kupitia mtandao wa kasi utakaotoa huduma bure kwa
wanafunzi kupitia maudhui ya Kidijitali kutoka Maktaba mtandao ya Mamlaka ya
elimu.
Vile vile Waziri wa elimu, Mkenda alisema; "Mpango huu utasaidia
kuongeza viwango vya ufaulu na ubora wa elimu, bila shaka utaweza kusaidia
kuimarisha vijana wetu".
Kwa upande wake Aneth Komba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya
elimu Tanzania alisema,program ya SmartWasomi inatekelezwa na wizara tatu
ambazo ni ile ya elimu,ofisi ya Rais Tamisemi pamoja na wizara ya Habari.
Alisema kuwa,lengo la mradi ni kuimarisha matumizi ya Tehama katika
ujifunzaji na ufundishaji na kwa kuanzia taasisi ya elimu imeanzisha maktaba
mtandao iliyowekwa vitabu vyote vya kinda na ziada.
Mkurugenzi huyo alisema,Kampuni ya Airtel Tanzania imeondoa gharama zote za bando na intaneti na hivyo maktaba mtandao inapatikana bila gharama ambapo matarajio ni walimu kuweza kutumia kuwasaidia wanafunzi na kupunguza changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni.









No comments:
Post a Comment