Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Jingu Jackson Jingu, akizungumza na Waandishi wa Habari Julai 18, 2024. Kushoto ni Kada wa chama hicho, Joseph Salum na kulia ni Katibu wa Chadema Jimbo la Singida Mjini Hamisi Nkua.
...................................
Na Mwandishi Wetu, Singida
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida kimelalamika viongozi wao ambao wametumwa na chama hicho Taifa kwa ajili ya zoezi la usajili na uandikishaji wa kidijitali kupata usumbufu na changamoto za kufuatiliwa na kutishwa na watu wanaozani kuwa ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotumia pikipiki zilizoandikwa ubavuni neon la SSH.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Jingu Jackson Jingu ametoa malalamiko hayo Julai 18, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa viongozi wao hao wamekuwa wakifuatiliwa na watu hao katika kila vitongoji na vijiji wanapopita kufanya usajili huo.
Jingu alisema lengo la mkutano huo ni kutaka kutoa rai kwa jeshi la polisi kuwa wawe makini wanapozifikisha taarifa hizo kwao waweze kusimamia misingi ya sheria na utawala bora wa nchi kama inavyotakiwa ili madai hayo wanayosema waweze kuyafanyia kazi kwa kuwasihi wenzao wa CCM wasije wakaleta hali ya taharuki na uvunjivu wa amani ambao unaweza kutokea kwani nao hawata kubali kuona hali hiyo ikiendelea kwa viongozi wao wakiendelea kufuatiliwa kwani kinachofanyika kipo kisheria kwa ajili ya kutimiza taratibu kwa ajili ya kufanya uchaguzi.
“Tunakuomba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida uone njia bora ya kuwashauri wenzetu wa CCM waache kutufuatilia tunapofanya ziara zetu ambazo zipo wazi na kuwa hakuna asiye jua kuwa tunauchaguzi ndani ya chama hivyo wachukue hatua pale inapobidi,” alisema Jingu.
Aidha Jingu aliomba jeshi hilo kuacha tabia ya kuwakamata viongozi wao na kuwafungulia kesi ambazo sio za lazima hivyo kuwapelekea usumbufu jambo ambalo alidai sio zuri na kuwa yaachwe na yasifanyike tena na kuongeza kuwa hata mahakama ilipowapa dhamana changamoto kubwa walioipata ni watendaji wa kata hawakuwa tayari kuandika barua za dhamana ambapo wanaiomba mahakama iwe inapokea malalamiko hayo ya watendaji kutowapa barua hizo.
Jingu alisema kuwa zoezi la usajili na uandikishaji kwa njia ya kidijitali linakwenda vizuri na kuwa ndani ya Mkoa wa Singida kichama ahitaji vurugu na mtu yeyote kiwe chama au taasisi yoyote wala jeshi la Polisi na wanachokihitaji kila jambo linalfanyika liwe wazi na wafanye shughuli zao za chama kwa uhuru kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza na si vinginevyo.
Kwa upande wake Joseph Salum ambaye ni kada wa CHADEMA Wilaya ya Iramba alisema kiongozi wa chama hicho kutoka Taifa ambaye anaongoza zoezi la usajili na uandikishaji kwa njia ya kidijitali naye alikumbwa na changamoto ya kukamatwa na polisi baada ya kiongozi mmoja wa kisiasa wa CCM kuagiza polisi wamkamate na hata alipoitwa kituo cha polisi kwa ajili ya kueleza makosa aliyofanya kiongozi huyo wa usajili kutoka Chadema alishindwa kufika .
Naye Katibu wa Chadema Jimbo la Singida Mjini Hamisi Nkua alisema anasikitishwa na tabia ilnayoendelea katika maeneo mbalimbali wilayani humo ya bendera za chama hicho zinaposimikwa kwenye ofisi za chama hicho na kwenye matawi yao kung’olewa na vijana wanaodaiwa kutumwa kufanya hivyo na viongozi ambao anadai ni wa CCM.
“Tunaliomba jeshi la Polisi kuliangalia kwa karibu jambo
hilo na ikiwezekana kwenda kuonana na
viongozi wa chama hicho ili kuzungumzia jambo hilo kwani vitendo vya namna
hivyo katika maeneo mengine ya nchi vimeweza kusababisha umwagaji wa damu.
Katibu wa Chadema Jimbo la Singida Mjini Hamisi Nkua. (katikati) akichangia jambo kwenye mkutano huo.







No comments:
Post a Comment