Kamati
ya Usimamizi wa Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria
ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) imekutana kwa ajili ya kupitia taarifa za
utekelezaji wa mradi huo.
Katika kikao
hicho
cha nne kilichofanyika leo Jumatatu
Julai 15, 2024 kimeongozwa
na Kaimu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais, Bw. Abdallah
Hassan Mitawi ambapo amesema mradi huo utaongeza
uwezo wa kitaasisi katika kuimarisha uzingatiaji wa sheria na
mifumo ya utekelezaji.
“Utekelezaji
wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira umekabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa rasilimali
watu na rasilimali
fedha katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya rasilimali mazingira
katika ngazi zote. Mradi huu umekuja na suluhisho la changamoto hizi” amesema Mitawi.
Wajumbe wa kikao hicho pia walipitia taarifa ya utekelezaji wa mradi
kwa mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na bajeti ya 2024/25, ambapo Mitawi amewahimiza kuusimamia vyema mradi
katika utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira
Pia
wajumbe wa kikao hicho walipata fursa ya kuipitia taarifa ya mpango wa
matumizi kwa mwaka wa fedha ulioanza Julai 2023 na kukamilika Juni 2024 kama
ulivyowasilishwa na Mratibu wa Mradi Bw. Richard Masesa.
Itakumbukwa kuwa Serikali
kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya
jitihada kadhaa za kulinda na kuhifadhi mazingira ikiwa ni pamoja na kuweka
Sera ya Kitaifa ya Mazingira (1997) pamoja
na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (2004).
Mradi
wa EMA unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Swedish (SIDA) unakusudia kushughulikia
changamoto kuu za mazingira na kuondoa vizuizi vya kisekta vilivyopo katika
Wizara na mamlaka maalumu
za kisheria na kuongeza wigo wa utendaji.
Mradi wa EMA unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC).







No comments:
Post a Comment