Na Dotto Mwaibale, Njombe
KIWANDA cha kuzalisha mipira ya mikono cha MSD kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe kinatarajia kuanza rasmi kuuza bidhaa zake kwa wadau mbalimbali hivi karibuni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji Februali 12, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari kimezalisha jozi milioni 2.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho leo kinachomilikiwa Bohari ya Dawa (MSD) kupitia kampuni yake tanzu ya MSD Medipham Manufacturing CO LTD, Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Shiwa Moshi, alisema kina uwezo wa kuzalisha jozi (pear) 10,000.
Mbali na kampuni tanzu kumiliki kiwanda hicho, inamiliki viwanda vingine viwili ambavyo vipo hatua za mwisho.
Viwanda hivyo no kiwanda cha kuzalisha bidhaa za pamba kilichopo Simiyu na Zengereni cha Pwani ambacho kitakuwa kinazalisha dawa
Kwa mujibu was Moshi, kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono milioni 86.4 sawa na asilimia 83 4 ya mahitaji ya nchi.
Nae Meneja Uhusiano Mkuu was MSD, Etty Kusiluka, , alisema tayari wanelekea kuanza kuuza bidhaa zake .
Alisema kabla ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho, MSD ilikuwa mdau
mkubwa wa kununua bidhaa hizo, kuuza na kuzisamba kwa wadau, ikiwemo hosptali,
vituo na zanahati.










No comments:
Post a Comment