Na Mwandishi Wetu, Manyoni
Kila ifikapo Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha Siku ya
kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakitetea, Kuupigania na
Kulinda Uhuru wa Tanzania. Siku hii pia
huambatana na Shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalumu za kuwaombea
Mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea Amani ya Nchi yetu Tanzania.
Mashujaa wetu walipambana kwa Hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya
Tanzania wakiwa katika Maeneo Mbalimbali, Walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani Maisha
yao kwa ajili ya Tanzania.
Uongozi na Menejimenti ya Wilaya ya Manyoni tunaungana na Watanzania wote
kuwakumbuka na kuwaombea kutokana na
kujali na kudumisha Misingi ya Amani ambayo matunda yake tunayaona mpaka sasa.
Misingi mizuri na imara iliyojengwa wasisi wa Taifa letu Baba wa Taifa,
Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere Na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na
Utulivu,huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote wa
Ndani au Nje. Amani iliyojengwa na
imepelekea wageni, wakimbizi na watalii kuifanya Tanzania kuwa kivutio
na kimbilio kwao.
Tuendelee kuienzi na kuilinda Amani ya Nchi yetu kwani Wapo wanaosema na
kufananisha Amani sawa na Yai mkononi
ambalo ukilivunja hautaweza kulinganisha kamwe lakini pia wengine wanasema
Amani haina bei na ikipotea haina soko
la kununua hivyo ni vema Tuitunze Amani yetu.
Wilaya ya Manyoni imeadhimisha siku hii kwa kushiriki Matembezi/ Mchakamchaka kwa pamoja
kufanya Usafi kuzunguka maeneo mbalimbali na Pia kuwasha mnara wa Mashujaa kama
Ishara ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi mashujaa wetu.













No comments:
Post a Comment