Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kukutanisha wadau zaidi ya 1000 kwa
ajili ya Mkutano wa kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za
uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika tarehe 9-10 Septemba,
2024 Jijini Dodoma.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo Agosti 26, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji amesema Mkutano
huo Viongozi watakaoshiriki Mkutano huu ni Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka
Wizara za Kisekta; Wakuu wa Mikoa; Wakuu wa Wilaya; na Wakurugenzi wa Halmashauri.
Aidha
amewataja wadau wengine kuwa ni pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali;
Mashirika ya Umma, Sekta binafsi, vyuo vya elimu ya juu na Asasi zisizo za
Serikali, Wakurugenzi kutoka katika mashirika ya Umma na wataalamu; Sekta
Binafsi.
Dkt.
Kijaji amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali za mazingira
ikiwemo uharibifu wa ardhi; uharibifu wa vyanzo ya maji; ukataji miti ovyo na
uharibifu wa misitu; upotevu wa makazi ya wanyamapori na bayoanuai ambazo
zimechangia kufifisha ustawi wa jamii na uchumi.
“Kwa
kutambua mchango wa wadau katika kuhifadhi na kusimamia mazingira na mabadiliko
ya tabianchi nchini, Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu Mkutano wa viongozi, wataalamu
na wadau wa hifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika tarehe
09 -10 Septemba, 2024 Jijini Dodoma” amesema Waziri Kijaji.
Ameongeza
Mkutano huo unalenga kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na usimamizi wa hifadhi ya
mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na fursa zilizopo
katika Biashara ya Kaboni; usimamizi wa
taka; mabadiliko ya tabianchi; nishati safi ya kupikia; upandaji miti na usimamizi
na uzingatiaji wa Sheria nchini.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kijaji amesema ni wajibu wa wadau mbalimbali kujitokeza katika kuunnga
mkono juhudi za Serikali katika kuzuia uharibu wa mazingira ikiwemo utegemezi
mkubwa wa kuni na mkaa kama chanzo cha nishati, kilimo kisicho endelevu,
utupaji taka ovyo, na ufugaji wa mifugo usiowiana na maeneo ya malisho.
Kwa mujibu wa Dkt. Kijaji ameeleza kuwa Mkutano huo unatarajia kutoa taswira na mustakabali wa hali ya mazingira na ushiriki wa wadau na taasisi mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi katika kukabiliana na hali ya uharibifu wa maizngira na mabadiliko ya tabianchi nchini.
(NA MPIGAPICHA WETU
0 Comments