MWEZESHI wa Mafunzo ya Ujasiriamali Mkoa wa Singida, Saimon Sirilo ametoa mafunzo kwa Timu ya Wanawake na Samia kutoka Halmashauri ya Itigi yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi.AJI wa Mafunzo ya Ujasiriamali Mkoa wa Singida, Saimon Sirilo ametoa mafunzo kwa Timu ya Wanawake na Samia kutoka Halmashauri ya Itigi yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari Sirilo alisema
mafunzo hayo ya siku moja yamelenga kuwajengea uwezo katika nyanja ya uchumi
ili waweze kujiimarisha zaidi kwa maslahi ya familia zao, jamii na Taifa kwa
ujumla.
Alisema wanawake hao wamefundishwa mambo kadhaa
ikiwemo fursa ya mkopo wa asilimia 4 inayotolewa na halmashauri ambayo inawahusu wanawake, Elimu ya Ujasiriamali kupitia dhana yake, Huduma kwa wateja, mauzo na masoko.
Aidha, Sirilo alisema pamoja na kupatiwa mafunzo hayo wanawakw hao wamekumbushwa kushiriki kujiandisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kushiriki kikamilifu uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu jambo litakalo mpa nguvu Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025.
0 Comments