........................................
Na Mwandishi Wetu
Wadau wa sekta ya usafirishaji wamempongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa
ya kuimarisha biashara nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dakimp International Ltd, Ally Said Sleyyum amesema
kuwa mazingira ya biashara yameboreshwa na hivyo kuwa chachu ya ukuaji wa
uchumi.
"Kwa muda mrefu, nimekuwa katika shughuli za biashara, haswa katika
sekta ya uchukuzi, nimeona mabadiliko makubwa," amesema Bw Sleyyum.
Amesema kuzinduliwa kwa treni ya umeme ya Standard Gauge Railway (SGR)
kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kutasaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la
wafanyabiashara kutoka nchi za Maziwa Makuu.
"Wateja wetu kutoka Mataifa ya Maziwa Makuu sasa watapata fursa ya
kutumia muda mfupi katika usafirishaji wa bidhaa zao kwa kutumia SGR,"
amesema Bw Sleyyum ambaye kampuni yake imekuwa ikitoa na kusafirisha mizigo
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha, amesema kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa mbalimbali
nchini utasaidia pia katika ukuaji wa uchumi.
Kulingana naye, katika kipindi kifupi kijacho, Tanzania itakuwa kinara wa
biashara katika ukanda wa maziwa makuu.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amebainisha kuwa, mazingira wezeshi yaliyowekwa na
serikali yamefungua milango zaidi ya kibiashara, hasa katika kuondoa urasimu na
ubabe kwa walipaji wa kodi.
"Zamani hali ilikuwa tofauti, mnadaiwa kodi kwa vitisho, leo hakuna
mambo hayo, TRA na sisi walipakodi tunajadiliana na kulipa kodi bila
vitisho," amefafanua.
"Kwa sasa hatuna mgogoro na TRA, tunashirikiana nao vizuri, mamlaka
imejirekebisha sana," Ameongeza.
0 Comments