MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA JAMHURI YA MSUMBIJI-MGENI RASMIN RAIS WA ZANZIBAR MHE.DKT. MWINYI

Subscribe Us

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA JAMHURI YA MSUMBIJI-MGENI RASMIN RAIS WA ZANZIBAR MHE.DKT. MWINYI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiangalia ngoma za Utamaduni wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji,baada ya kumalizika kwa uwekaji wa Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa Viwanja vya Matora, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Msumbiji  yaliyofanyika tarehe 7-9-2024, na (kushoto kwa Rais) mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi.
(Picha zote na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Mshumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akiwa na Mkewe Mama Isaura Nyusi, wakisalimiana na Wananchi baada ya kumalizika kwa hafla ya uwekaji wa Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa katika viwanja vya Matora Msumbiji .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akiwa na Mkewe Mama Isaura Nyusi, wakiondoka katika uwanja wa mpira wa Matora baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji iliyofanyika katika uwanja huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mgeni rasmin katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Msumbiji, akipata maelezo ya picha mbalimbali za historia ya ukombozi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, wakati akitembelea maonesho hayo katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mgeni rasmin katika Sherehe za Maadhimisho ya Miako 50 ya Ushindi wa Msumbiji, akimsikiliza mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akielezea picha mbalimbali wakati akitembelea maonesho  hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji .
BAADHI ya Askari walioshiriki katika mapambano ya kuikomboa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, wakishiriki katika gwaride maalumu la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji wakipita katika jukwaa kuu la Viongozi katika uwanja wa mpira matora  Msumbiji, wakati wa maadhimisho hayo .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji.
WANANCHI wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji wakimsikiliza mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji .
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji.

Post a Comment

0 Comments