WAHITIMU WA CHUO CHA PASIANSI NI HAZINA ADHIMU KWA MALIASILI NA UTALII NCHINI.

Subscribe Us

WAHITIMU WA CHUO CHA PASIANSI NI HAZINA ADHIMU KWA MALIASILI NA UTALII NCHINI.

Na Sixmund J. Begashe

Sekta binafsi wanaojishughulisha na uhifadhi wa wanyamapori au biashara zinazoendana na uhifadhi wa wanyampori zimetakiwa kutoa nafasi za ajira kwa vijana waliohitimu katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi ili kuongeza tija katika shughuli za Uhifadhi na Utalii kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wanachi maendeleo kupitia Maliasili na Utalii.

Wito huo umetolewa kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula Jijini Mwanza, kwenye mahafali ya 59 ya Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.

Mhe. Kitandula amesema wahitimu wa mafunzo ya Uaskari wa Wanyamapori na Himasheria, Uongozaji na Usalama wa Watalii na mafunzo ya muda mfupi kwa askari wa vijiji kutoka maeneo mbalimbali ni azina muhimu kwa Uhifadhi na Utalii hivyo ni vyema ikatumika vizuri kwa maslai mapana ya Taifa.

Aidha Mhe. Kitandula anetumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wafadhili wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa kulipia ada za masomo na mahitaji mengine iliyofanikisha kuhitimu mafunzo kwa baadhi ya wanachuo hao.

Akitoa Taarifa ya mafunzo hayo Mkuu wa Chuo hicho Bw. Jeremiah Msigwa amefafanua kuwa kati ya wanachuo 374 waliodahiliwa,Wanachuo 354 wamepewa vyeti vya kuhitimu mafunzo kulingana na viwango (grade) mbalimbali vya ufaulu wakiwemo wanachuo 222 wa kozi ya BTCWLE, 70 wa kozi ya TCWLE; 34 wa kozi ya BTCTGTS na 04 wa kozi ya TCTGTS.

Post a Comment

0 Comments