Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhe Mhandisi Maryprisca Mahundi
ameanza Ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Mkoa wa Mbeya kwa gharama zake zaidi ya
Milioni 70 . Lengo la kujenga nyumba hiyo ni kutekeleza agizo la Mwenyekiti wa
UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda la kuzitaka kila Wilaya na Mkoa kujenga nyumba za
Makatibu wa UWT pamoja na kuanzisha Vitega Uchumi.
Aidha Mhandisi Mahundi amewataka wadau wengine kujitokeza kujenga nyumba
nyingine kwa UWT Kwani nafasi ipo katika kiwanja kilichopo ForestMpya Jijini
Mbeya.Katika hatua nyingine amepongeza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya pamoja
na viongozi wake Ndugu Edina Mwaigomole kwa kusimamia vyema mradi huo.







No comments:
Post a Comment