Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akiongoza kikao cha cha kwanza cha robo ya nne cha baraza la madiwani kilichoketi kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye kata katika kipindi cha 2023/ 2024 kilichofanyika Septemba 10, 2024.
............................................
( Imeandaliwa na Dotto Mwaibale / Philemon Solomoni )
0754-362990
MKURUGENZI
wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia ameshiriki baraza la madiwani la
manispaa hiyo kwa mara ya kwanza tangu amehamishiwa Singida ambapo ametumia
nafasi hiyo kujitambulisha na kuomba kupewa ushirikiano katika utendaji wa kazi.
Kataraia
aliomba ushirikiano huo katika kikao hicho cha kwanza cha robo ya nne cha
baraza la madiwani kilichoketi kwa ajili ya kupitia taarifa za utekelezaji wa
shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye kata katika kipindi cha 2023/ 2024 kilichofanyika ukumbi wa
mikutano wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
“Kwanza
kabisa napenda nijitambulishe kwenu likiwa baraza la kwanza kushiriki nikiwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida waheshimiwa wajumbe naitwa Joanfaith John
Kataraia ndio Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida ninapenda kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kunipa kibali cha kuijenga na kuiendeleza Manispaa yetu ya Singida,”
alisema Kataraia.
Pia Kataraia
alitumia nafasi hiyo kumshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kumuamini na kuendelea kutumika katika nafasi ya ukurugenzi.
“Mheshimiwa mwenyekiti
wa kikao hiki Mstahiki Meya napenda kukushukuru pamoja na watumishi wote wa Manispaa
ya Singida kwa mapokezi makubwa mlionifanyia na ushirikiano mlionipa naomba
muuendeleze ili tuweze kuitengeneza Manispaa yetu vizuri,” alisema Kataraia.
Akizungumza
katika kikao hicho, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Yagi Kiaratu alitoa angalizo
kwa watendaji hao kwa kuwaambia kuwa kila ngoma inachezwa kwa midundo yake
hivyo waachane na midundo iliyopita na kuanza milio mipya ‘tune’ ili Kataraia
asije akawaona ni watu wa tofauti kwa kuwa wanacheza midundo ya zamani ambapo
aliwaomba watendaji hao kwenda na kasi ya utendaji wa kazi wa mkurugenzi huyo.
Kiaratu naye
kwa nafasi yake aliwaomba madiwani na watumishi wa Manispaa ya Singida kumheshimu, kumsikiliza na kumpa ushirikiano wa kutosha ili Manispaa ya Singida iendelee kupaa
kimaendeleo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Singida, Lusia Mwiru alimueleza
Kataraia kuwa wilaya hiyo inaongozwa na madiwani wote 18 wanaotokana na CCM
wakiwemo na wa viti maalumu pamoja na wabunge.
“Hivyo ujue
sisi hapa tunaimba wimbo mmoja pia nataka kukuambia kwamba tunaushirikiano
mzuri sana baina ya Serikali na CCM hususani ofisi yako na hawa watendaji
unaowaona hapa tunaimba wimbo mmoja na sisi tunaamini na wewe utakuwa mwenzetu,”
alisema Mwiru.
Mwenyekiti
huyo alisema alibahatika kuwa mmoja wa wenyeviti wa chama hicho waliokwenda
Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mafunzo ambako alikutana na baadhi ya
wenyeviti wa chama hicho wa Mkoa wa Morogoro akiwepo Katibu wa Mkoa ambao
walimueleza Kataraia kuwa ni mchapa kazi mzuri na Manispaa ya Singida
imebahatika hivyo wana kila sababu ya kumshukuru Rais Samia kwa kumuamini na
kumuhamishia Singiga.
TAZAMA VIDEO HAPA
0 Comments