*Mwenyekiti
wa kijiji asema ni matunda ya oparesheni maalumu.
*DC Shaka
asisitiza mkakati wa kujenga maelewano kwa makundi hayo.
Na MWANDISHI
WETU
WATU 12
wakazi wa Kijiji cha Malangali, Kata ya Tindiga wilayani Kilosa, Mkoa wa
Morogoro, wanashikiliwa Polisi na wengine wanane wanaendelea kusakwa wakidaiwa
kuhusika na vurugu za wafugaji na wakulima.
Akizungumza
katika mkutano uliotishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka,
kijijini hapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Malangali, Seleman Mapala, alisema
vurugu hizo zilitokea Septemba 8, mwaka huu baada ya wafugaji kudaiwa kuingiza
mifugo katika mashamba ya wakulima.
Mapala
alisema baada ya wafugaji kitendo hicho, inadaiwa wakulima waliamua kukamata
mifugo na kuijeruhi kwa kukaikata kwa kitu chenye ncha kali jambo
lililosababisha kuibuka kwa vurugu na uvunjifu wa amani.
Alieleza
kwamba, kwa zaidi ya wiki tatu sasa
kumekuwepo na mkakati wa wilaya hiyo kudhibiti mifugo na wafugaji wakorofi
inayotekelezwa na vyombo vya ulinzi na usalama chini usimamizi wa Mkuu wa
Wilaya hiyo, Shaka.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti huyo, operesheni hiyo imeonesha mafanikio makubwa katika kipindi
kifupi tangu ilipoanza kutekelezwa.
"Kuna
kikundi cha watu baada kuona mkakati huu unafanikiwa wanataka kuwaaminisha
wananchi kuwa hili wanalifanya wao, hivyo wemewashawishi vijana wadogo nao
kujihusisha katika ukamataji mifugo kinyume na utaratibu.
“Lengo lao ni kujijenga kisiasa jambo ambalo limesababisha kuchochea uvunjifu wa amani kijijini kwetu," alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kata ya Tindiga, Filimon Karao, akizungumza katika mkutano huo, aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa wamoja na kuheshimiana kwa kuwa wao ni ndugu na baaadhi ya wafugaji wamezaliwa katika eneo hilo.
"Tunashukuru sana jitihada za DC (Mkuu wa Wilaya) kutaka kutuunganisha kuwa wamoja tuishi kwa upendo na mshikamano, kinachosikitisha ni kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa hususan upizani kutaka kutumia kivuli chake kuaminisha watu mambo ambayo hawakuyafanya.
“Lengo lao
ni kujitafutia umarufu na kutaka kusababisha umwagaji damu baina wakulima na
wafugaji, wanawashawishi vijana wadogo kuyafanya hayo" alisema.
Kwa upande
wake Shaka, alisema serikali imejipanga vyema na haitaruhusu jambo lolote la
uvunjifu wa amani au umwagaji damu kwa kisingizio cha mgogoro wa wakulima na
wafugaji.
"Nimekuwa
nikisema mara kwa mara wako watu ni wanufaika wa migogoro hii, hivyo wakiona
jitihada zozote za serikali kutaka kulimaliza kwao ni shida, operesheni
tuliyoianzisha inakwenda vyema, yeyote atakayetaka kukwamishana atakumbana na
mkono wa sheria.
"Hiki
kinachofanyika ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan
kutaka wafugaji na wakulima waishi pamoja kwa upendo na mshikamano bila
kurudishana nyuma kiuchumi na kuleta uvunjifu wa amani nchini, hivyo kazi kubwa
inayofanyika ni kujenga ustawi wa makundi hayo na kukomesha, kumaliza kabisa
changamoto hiyo," alisema.
Alisema
waliohusika na vurugu hizo wanaendelea kusakwa kwa lengo la kuchukuliwa hatua
zaidi za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani bada ya upepelezi wa polisi
kukamilika.
Mkuu wa
Oparesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Mihayo
Msikhela alisema jeshi hilo halitamvumilia yeyote atakaye vunja sheria.
0 Comments