SPIKA wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt.Tulia Acksonamewataka Mama lishe na wananchi kutumia nishati safi ya gesi ili kutunza mazingira na kuokoa muda wa shughuli za kiuchumi huku akisisitiza kuwa umefika wakati wa kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Ameyasema
hayo Septemba 30,2023 akiwa na wadau wa nishati safi ya kupikia kutoka
Kampuni ya Gesi ya Oryx baada ya kwenda katika Mgahawa uliopo Mtaa wa
Uyole jijini Mbeya ambapo aliamua kupika chakula kwa gesi kwa ajili ya kuuza
kwa wananchi kama sehemu ya kuonesha mfano kwa mama lishe na baba lishe kupika
kwa gesi.
Amesema
lengo la kuhamasisha watanzania kupikia nishati safi ni kuunga mkono kampeni ya
Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi
badala ya mkaa na kuni.
Kwa
upande wake Meneja wa Miradi ya Nishati Safi ya kupikia kutoka Kampuni ya Gesi
ya Oryx Peter Ndomba amesema wamekuwa wakisaidia makundi mbalimbali yakiwemo ya
Mama na Baba Lishe kupata nishati safi ya kupikia na tangu kwa kampeni ya
kuhamasisha nishati safi wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake zaidi ya 70,000.
"Oryx
tunafahamu dhamira ya Rais DK.Samia Suluhu ni kuhakikisha katika kipindi cha
miaka 10 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia na
Kampuni yetu imeibeba ajenda hiyo kwa vitendo.
"Leo
hii tupo hapa tumeungana na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Mbeya kupitia taasisi ya Tulia Trust tuumekuwa naye katika jitihada
hizi za nishati safi.Dk.Tulia ameamua kwenda moja kwa moja na amekuwa mfano na
kielelezo cha matumizi ya nishati safi kwa wananchi,"amesema.
Amefafanua
akiwa na Dk.Tulia wameshuhudia mama lishe wengi wanatumia kuni na mkaa,hivyo
kuamua kwenda kwa mama Lishe na kupika kwa gesi maana yake ni kufikisha ujumbe
kwa kundi kuona haja ya kutumia nishati safi ya kupikia.
"Dk.Tulia
amekuwa mfano amepika mwenyewe kwa gesi na hii kwetu Oryx imetufurahisha
sana kupata kiongozi kama huyu ambaye amemua kuwa mfano wa moja kwa moja kwa
wananchi. Ni alama kubwa sana kwamba hili jambo linawezekana.
"Watu
wengi watabadilika, kwani tunafahamu makundi mbalimbali yakiwemo ya Baba na
Mama Lishe ambao tunaona kila siku wako katika kuni na mkaa maisha yao yako
hatarini.Tunaambiwa makundi yanayofanya shughuli za kupika yako hatarini
zaidi.Watanzania zaidi ya 33000 wanafariki kila siku kwasababu ya kutumia kuni
na mkaa .
"Mama
Lishe na Baba Lishe maisha yao ni moto na kuni hivyo tukianza na kundi hili
tunaweza kuokoa Watanzania ,kwa hiyo tunashukuru kwa Tulia Trust pamoja na
vyombo vya habari kwa kupeleka taarifa kwa umma ili kila mmoja aifuate . Ndani
ya wiki tatu zilizopita hapa Mbeya tumetoa mitungi ya gesi 1000 kwa mama Lishe
na Baba Lishe." 










No comments:
Post a Comment