……..
Na Mwandishi Wetu,New
York ,Marekani
Katibu Mtendaji wa
Tume ya Taifa ya UNESCO ya Tanzania, Prof. Hamisi Malebo amesema kuwa Tanzania
haina ardhi ya Mababu ,Ardhi ya Makabila pamoja na ardhi ya kimila.
Akijibu taarifa ya
Mwandishi katika mada ya “Watu wa Asili wanaohamishwa toka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine “Amesema Profesa Malebo na kuongeza taarifa iliyotolewa
haijazingatia sheria za ndani za nchi jambo linalosababisha upotoshaji”
Profesa ameyasema
hayo katika mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uunaendelea hadi
jijini New York nchini Marekani.
Katika mkutano huo
kulikuwa na Kikao cha Kamati ya tatu ya Masuala ya Watu wa Asili kilichofanyika
15 Oktoba 2024 wakati wa uchangiaji wa taarifa iliyosomwa na Mwandishi Maalum
wa Umoja wa Mataifa wa Masuala na Haki za Watu wa Asili, Bw. José Francisco
Calí Tzay, aliibua suala Tanzania kuhamishwa sehemu moja kwenda nyingine.
Prof. Malebo
alisisitiza kuwa msimamo wa Serikali kuwa makabila yote Tanzania yana haki sawa
mbele ya sheria na hakuna kabila lenye haki zaidi ya mengine.
Aidha amesema wakati
akichambua jinsi Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Masuala na Haki za
Watu wa Asili, Bw. José Francisco Calí Tzay, alivyoelezea masuala ya ardhi na
watu wa asili aliuelezea mkutano huo kuwa Mwandishi hakuzingatia uhuru wa Nchi
Wanachama.
Prof. Malebo alihoji
juu ya Mwandishi ni kwa nini anaripoti masuala ya umiliki wa ardhi huku akifumbia
macho na kupuuza sheria za ndani za nchi husika.
Prof. Malebo
alisisitiza msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa nchi yetu haina ardhi ya
mababu wala ardhi ya makabila au ardhi ya kimila.
Profesa Malebo
alibainisha kuwa katika sheria za Tanzania hakuna ardhi ya mababu wala ardhi ya
makabila au ardhi ya kimila na akataka Mwandishi na Jumuiya ya Kimataifa
itambue kuwa masuala hayo hayamo katika mfumo wetu wa sheria.
Alifafanua pia
kinachoendelea katika eneo la Ngorongoro ni kuhama kwa hiari kufuatia wananchi
kuelimishwa na wao wenyewe kupewa nafasi ya kuridhia na kujiandikisha kwa hiari
kwa wakazi wanaotaka kuhama kutoka katika eneo hilo ili kupisha uhifadhi.
Prof. Malebo
aliukumbusha mkutano huo juu ya mfumo mkuu wa Ikolojia wa Serengeti-Mara, ambao
ni mfumo pekee uliosalia wa kuhama wanyamapori na haupo katika eneo lingine
duniani.
Katika Mkutano huo
Prof. Malebo alisisitiza kwamba, Tanzania ina mikoa 31 ya kiutawala,
ikijumuisha 26 ya Bara na Mitano ya Zanzibar na kulingana na Katiba na Sheria
za nchi, kabila lolote Tanzania linaweza kuishi popote nchini.
Ailitolea mfano
kabila la Wamasai ambao kwa sasa wapo na wanaishi katika mikoa 22 ambayo ni 71%
ya mikoa yote nchini Tanzania, ambako wanaishi na kutekeleza maisha yao ya
kifugaji na kitamaduni.
Amesema Sera ya sasa
ya ardhi inatoa haki ya kupata na kumiliki ardhi popote nchini ikiwa na dhamana
ya kikatiba ya raia wake kusafiri na kuishi kwa uhuru ndani ya nchi.
Amesema Sera hiyo
imewafanya wananchi wa Tanzania kuishi kwa amani na kwa maelewano.
Prof. Malebo
aliongeza kuwa suala la ardhi ya mababu au ardhi ya asili haitumiki kwetu na
wala haihuusu Tanzania kutokana na ukweli wa sheria yetu nchini
Prof. Malebo
alihitimisha kwa kumhabarisha Mwandishi Maalum kuwa kuna msemo mmoja nchini
Tanzania unaosema, ‘Kuona ni kuamini’ na akamhoji ni lini atatembelea Tanzania,
ardhi ya Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, na Zanzibar ambapo amemuhakikishia
atakuta zaidi ya makabila 123 yanayoishi pamoja na kuishi kwa maelewano na
amani.
Katika taarifa
iliyotolewa na mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Prof.Malebo amemtaka
kutembelea Tanzania hapo ndipo atashuhudia hali halisi badala ya kutegemea
uvumi na propaganda anazopelekewa ambazo hazina msingi wala ukweli
Mkutano huo kwa Tanzania ulihudhuriwa Zuleikha Tambwe, Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Prisca Kasalama Msaidizi wa Afisa Kamati ya Tatu wote kutoka katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.









No comments:
Post a Comment