RC SINGIDA AOMBA WAKUU WA VYUO KUANZISHA SILABASI ZA MALEZI YA WANAFUNZI, AUKUMBUKA UNYAGO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 15 October 2024

RC SINGIDA AOMBA WAKUU WA VYUO KUANZISHA SILABASI ZA MALEZI YA WANAFUNZI, AUKUMBUKA UNYAGO

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ambaye alikuwa mgeni rasmi akionesha nyaraka za uzinduzi wa kampeni hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida,  Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo cha Ualimu na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) vyote vya Singida alipokuwa akizindua Kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharikiwa iliyoanzishwa na Jeshi la Polisi nchini kupitia Dawati la Jinsia na Watoto.

........................

Imeandaliwa na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amewataka wakuu wa vyuo kuanzisha silabasi za malezi kwa wanafunzi kwenye vyuo vyao ili kutoa elimu ya kuwajenga kimaadili.

Dendego ametoa ombi hilo Oktoba 15, 2024  wakati akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida,  Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo cha Ualimu na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi.

FDC vyote vya Singida alipokuwa akizindua Kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharikiwa iliyoanzishwa na Jeshi la Polisi nchini kupitia Dawati la Jinsia na Watoto.

“Nawaombeni anzisheni silabasi za malezi ya wanafunzi  zitasaidia kuwajenga kimaadili, zamani yalikuwepo mafunzo yaliokua yakitolewa kwa Wasichana ambayo yalijulikiana kama unyago na kwa wavulana yalikuwa yakiitwa jando mafunzo hayo yaliyawajenga vijana kimaadili lakini leo hii hayapo tena,” alisema Dendego.

Alisema uanzishwaji wa kampeni hiyo sio jambo dogo  inakwenda kukabiliana na mambo mabaya yanayotokana na utandawazi na maendeleo yanayotokana na teknolojia.

Dendego alisema zamani mtoto alikuwa akilelewa kuanzia ngazi ya baba, mama, mwalimu  na majirani lakini leo hii mtu hawezi kumkanya mtoto wa mtu mwingine na ndio sababu nyingine kubwa ambayo inachangia kumomonyoka kwa maadili.

Alisema kupitia utandawazi baadhi ya vijana wamekuwa wakikosa adamu hata kufikikia hatu ya  kumtuka Rais licha ya kufanyiwa mipango mizuri ya maendeleo.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka vijana kuacha tabia ya kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao za maisha kwa kuzingatia kuwa bado ni wategemezi kwa kila kitu kutoka kwa wazazi wao.

“Ukitaka kula nanasi unahitaji kuwa na nafasi na ukilila  kwa pupa huwezi kulila hivyo zingatieni masomo yenu,” alisema Dendego.

Aidha Dendego aliwaambia wanafunzi hao kuwa miaka mitatu ya chuoni sio mingi iwapo watafuata maelekezo ya walimu wao na kikubwa zaidi wasiache kumuomba Mungu kupitia vipindi vya dini vinavyofanywa kila wiki katika vyuo vyao.

Aliwaambia vijana hao kuwa wigo wa ulinzi wa maisha ya vijana hao wanaowenyewe hivyo wasitegemee kusaidiwa na mtu mwingine.

Dendego alisema siku hizi vifo vingi ni vya vijana na hiyo inatokana na changamoto mbalimbali akitolea mfano ukienda mabakurini na kuangalia umri wa vijana waliofariki wengi wao ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1980, 1990 na 2000.

Mhe. Dendegu aliwataka vijana kutumia simu zao kwa ajili ya kutangaza mambo mazuri ya Tanzania na kueleza kuwa anapoiona Tanzania jinsi ilivyopendelewa ni kama bustani ya Hedini ambayo ina vitu vyote kauanzia ardhi, bahari, wanyama, madini, chakula na vingine vyote na kusisitiza kuwa watanzania hatuna nchi nyingine mbadala wa Tanzania ambayo tunaweza kuikimbilia.

Dendegu pia alitumia uzinduzi huo kuwataka vijana hao kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowataka wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakapo wadia ambao utafanyika hivi karibuni.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mayunga Mayunga alisema mwaka 2006 jeshi la polisi lilifanya mapinduzi makubwa ya utendaji wake wa kazi na kuwa wakisasa na uweledi na kuanzishwa kwa polisi jamii na Dawati la Jinsia na watoto.

Mayunga aliwaambia vijana hao kuwa wakati wote wanapsawa kuacha kujiingiza katika vitendo vyote ambavyo vinaweza kuwaingiza kwenye changamoto mbalimbali na kuwa mategemeo yao makubwa yawe ni kupata mafanikio.

Aliwataka vijana hao kuacha kujiingiza katika vitendo vya ulevi, ngono zembe, matumizi ya aina zote za dawa za kulevya, kupenda vitu vya anasa na starehe na kuwategemea wafadhili ambao watawawezesha kupata fedha za kufanyika mambo hayo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida, Flora Lemnge alilishukuru jeshi la polisi kwa kuanzisha kampeni hiyo ambayo ni muhimu kwa wanafunzi hao na kueleza kwamba inakwenda kuchochea mambano dhidi ya vitendo vyote vya ukatili kwa wanafunzi hao.

Alisema katika vyuo hivyo kila darasa na hosteli yupo kiongozi wa dawati wa jinsia ambaye amekuwa akishughulikia vitendo hivyo na kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya mikutano miwili ambayo wamekuwa wakikutana na wanafunzi kwa ajili ya kuwajenga kimaadili ambayo imekuwa sanjari na michezo mbalimbali.

Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Singida, Salome Chomete na Abdi Imamu kutoka TIA Singida wakizungumzia kampeni hiyo walisema itakwenda kuchagiza jinsi ya kumaliza kama sio kupunguza vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vyuoni na kuwa elimu walioipata wanakwenda kuipeleka kwa wenzao ambao hawakubahatika kuipata.

“Wanafunzi wengi wanapofika kuanza masomo wanakuwa na maadili mazuri na uvaaji wa nguo wenye staha lakini wakisha kaa miezi kadhaa wanabadilika na kuanza kuvaa nguo za ajabu hivyo naamini kupitia kampeni hii itawabadilisha,” alisema Imamu.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulianza kwa maandamano yaliyohusisha wanafunzi wa vyuo mbalimba vilivyopo mkoani Singida yalioanzia Uwanja wa Bombadia na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA), Kampasi ya Singida, ambako zilitolewa hutuba za kuwajenga wanafunzi masuala ya maadili na burudani ya igizo, shairi na wimbo wa kizalendo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma.

Maandamano ya jeshi la polisi Mkoa wa Singida na wanafunzi wa vyo hivyo yakielekea Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida kwa ajili ya uzinduzi wa kamapani hiyo.

Mlezi wa Wanafunzi wa TIA Kampasi ya Singida, Ambene Kajula akiongoza itifaki ya kukaribisha wageni wakati wa kampeni hiyo.

Maandamano yakifanyika.

Heshima ya saluti ikitolewa wakati wa kuimba wimbo wa Taifa

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,Kamishna Msaidizi wa Polisi  (ACP) Mayunga Mayunga akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kaimu Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida, Flora Lemnge, akizungumza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego akipokea maandamano hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego akiingia ukumbuni baada ya kupokea maandamano hayo.
Maafisa wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Maafisa wa Jeshi la Magereza na Polisi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.
Viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida wakiwa kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Jamii, Mkoa wa Singida, ASP. Hamisi Muungwana,  Mkuu wa Oparesheni Mkoa wa Singida, ACP Majura na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Singida, 
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwanafunzi wa TIA Singida, Abdi Imamu akizungumzia uzinduzi huo.
Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Singida, Salome Chomete, akizungumzia kampeni hiyo.
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida wakiandamana wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
Viongozi wakiwa meza kuu.
Taswira ya uzinduzi wa kampeni hiyo. 

Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Singida wakiigiza igizo la kuzingatia maadili



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad