.................................
Na Mwandishi Wetu, Lindi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepeleka fedha za ujenzi wa
barabara mkoani Lindi na amemwagiza Meneja wa TANROADS wa mkoa huo, Mhandisi
Emil Silas Zengo ahakikishe barabara ya Kata ya Milola inawekwa lami mapema
iwezekanavyo.
Amefikia hatua hiyo baada ya Mhandisi Zengo kukiri kuwa walishapokea fedha
kiasi cha sh.bilioni 3.5 ambazo zililenga kujenga barabara ya Milalo Centre
yenye urefu wa kilometa nne, kujenga mitaro na kuweka taa za barabarani.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jioni (Ijumaa, Oktoba 18, 2024) wakati
akizungumza na mamia ya wakazi wa kijiji cha Milola, kwenye mkutano uliofanyika
kwenye senta ya Milola, kata ya Milola, wilayani Lindi.
Mhandisi huyo amesema Jumatatu ijayo (Oktoba21, 2024), wataalam wataenda
kwenye kata hiyo ili waweze kuanza kazi ya usanifu na hatua nyingine za msingi
zitaendelea ili baada ya mwezi mmoja, mkandarasi aanze kazi.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Rais Samia imekwishatoa sh.
bilioni 1.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali kwenye sekta za elimu na maji.
Waziri Mkuu amesema pia atafuatilia ahadi za Serikali kuhusu ujenzi wa
vituo vya afya vya Milola na Rutamba ili kazi hiyo ianze mara moja kwani maeneo
hayo yana idadi kubwa ya watu.
Alikuwa akitoa ufafanuzi wa hoja iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Mchinga,
Salma Kikwete ambaye aliomba ahadi ya Serikali ya ujenzi wa vituo hivyo
ifuatiliwe ili kuwanusuru wananchi hao na adha ya kukosa huduma bora za afya
kwani hivi sasa wanatibiwa kwenye zahanati.
Mkutano ukiendelea.









No comments:
Post a Comment