..................................
Na Mashaka Kibaya Tanga.
KAMPUNI ya Simba Supply Chain Solutions Ltd imekabidhi Kompyuta 48 na Vifaa
vya kuunganishia kwa Maktaba ya Kidijitali katika wilaya ya Muheza ili kuhakikisha watoto wanapata nyenzo sahihi
za kujifunzia, hivyo kwenda sambamba na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia.
Hayo yamebainika Jana kwenye ziara ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Doto Biteko aliyoifanya wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Taarifa hiyo imetoka Jana mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Terminal Operation
Manager wa Kampuni ya Simba Supply Chain Solution Ltd Ramadhan Hussein, alisema
katika kuendeleza mkakati wa kuwa karibu na jamii Kampuni yao imetoa Komyuta 48
na Vifaa vya kuunganishia ili kuwawezesha watoto kupata nyenzo za kujifunzia
hivyo kwenda sambamba na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia .
"Katika kuendeleza mikakati yetu ya kuwa karibu na jamii leo
tunashiriki hafla hii ya kuzindua Maktaba ya Kidijitali yaani Digital Library
ikiwa na kauli mbiu "Mtoto wa leo Samia wa Kesho".Katika kuunga mkono
kupitia Kampuni hii ya Simba Supply Chain Solutions Ltd umetoa Kompyuta 48 na
Vifaa vya kuunganishia"alisema Meneja huyo wa uendeshaji.
Aidha Meneja huyo Simba Supply Chain Solutions ltd amesema kwamba,ni
matumaini yake kuwa Vifaa hivyo vitatumika vyema ili kusaidia watoto hao na watu
wengine kupata elimu na maarifa zaidi ili kufikia malengo yao ya maisha na
hivyo kusukuma mbele maendeleo ya nchi.
Pamoja na kukabidhi msaada huo, Kampuni hiyo pia inaendesha kampeni ya utunzaji mazingira kwa kuotesha miti 23,000 katika Mkoa wa Tanga ambapo Juni 5 mwaka huu kampeni hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Salha Burian Shule ya Msingi Pande iliyopo Wilaya ya Mkinga.
Kampuni ya Simba Terminal Supply Chain Solutions ltd ni moja ya Kampuni
zilizopo chini ya Simba Bingwa Group unatoa huduma shirikishi za kibandari
kwenye bandari zilizopo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA.
Kampuni hiyo inajihusisha na umiliki,uwekezaji na uendeshaji biashara ya
kutoa huduma ya kupokea mizigo,kuhudumia kwa kufungasha,utunzaji wa mizigo na
usafirishaji mizigo.
Kupitia Mamlaka ya usimamizi wa Bandari, Kampuni ya Simba Terminal imekodisha eneo la Bandari ya Dar es Salaam na Tanga kwa ajili ya kuhudumia mizigo hiyo ambapo mpaka sasa Simba Terminal imefanikiwa kuleta Meli nane (8) zenye shehena mbalimbali katika Bandari ya Tanga.









No comments:
Post a Comment