Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida wakishusha maboksi yenye mashuka na mipira ya kujifungulia Wajawazito ambayo walitoa msaada ikiwa ni moja ya tukio lao kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.Habari Picha Dotto Mwaibale na Solomon Philemon
WAKATI
Tukielekea Wiki ya Huduma kwa Wateja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa
wa Singida limeanza kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya uzazi salama kwa mama na
mtoto.
Kaimu Meneja
wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Boniface Shitindi amesema wakiwa
wanaelekea wiki ya huduma kwa wateja wameamua kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Sindida kwa ajili ya kutoa msaada wa mashuka na mipira ya kujifungulia
wajawazito.
“Moja ya
Sera ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan inahimiza suala zima la uzazi salama kwa mama na mtoto na sisi
leo kama Shirika tumeamua kuja katika Hospitali hii kuunga mkono sera hiyo kwa
kutoa mashuka na mipira ya kujifungulia wajawazito,” alisema Shitindi.
Alisema
walichagua kwenda kutoa usaada huo katika hospitali hiyo ikiwa ni moja ya kutoa
shukurani zao kwa wateja wao kwa kuadhimisha wiki hiyo kwa kufanya hivyo.
Aidha,
Shitindi alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja wao kwa kuliamini shirika hilo
na kulipa nafasi ya kuwahudumia kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha ambapo pia
aliwahimiza waendelee kufurahia huduma yao ya umeme kwa kutumia nishati hiyo
safi kwa matumizi mbalimbali ikiwamo kujilinda kiafya na kutunza mazingira.
Kwa upande
wake Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo, Lovenes Nyange akizungumza kwa niaba ya
uongozi wa hospitali hiyo alitoa shukurani za dhati kwa Tanesco Mkoa wa Singida
kwa msaada huo.
Nyange alitumia
nafasi hiyo kulishukuru shirika hilo kwa huduma nzuri ya nishati ya umeme wanayoitoa
katika hospitali hiyo na mkoa mzima wa Singida ambapo aliyaomba mashirika,
taasisi zingine za Serikali,watu binafsi na wadau mbalimbali kuiga mfano wa
Tanesco kwani kuna maeneo mengi
hospitali hapo yanayohitaji msaada na kuwa Serikali peke yake haiwezi
kukidhi mahitaji yote ya wagonjwa.
Wafanyakazi wa shirika hilo wakishusha mashuka hayo kutoka kwenye gari.
Kaimu Meneja wa shirika hilo, Mhandisi Boniface Shitindi, akimkabidhi mashuka hayo Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Lovenes Nyange. Wengine ni wafanyakazi wa shirika hilo.
Kaimu Meneja wa shirika hilo, Mhandisi Boniface Shitindi, akimkabidhi mipira ya kujifungulia Wajawazito,Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Lovenes Nyange. Wengine ni wafanyakazi wa shirika hilo.
Kaimu Meneja wa shirika hilo, Mhandisi Boniface Shitindi (kushoto), Afisa Uhusiano na Uuduma kwa Wateja (TANESCO) mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo na Afisa wa shirika hilo Siatu wakitandika shuka katika moja ya kitanda cha wagonjwa kwenye hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa shirika hilo wakitoka kukabidhi msaada huo.
Wafanyakazi wa shirika hilo wakionesha furaha zao baada ya kukabidhi msaada huo.
Kaimu Meneja wa shirika hilo, Mhandisi Boniface Shitindi, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo.

















No comments:
Post a Comment