Waziri Mkuu
...........................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa
kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta
ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi.
Amesema kuwa maboresho hayo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki yatasaidia
kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya karatasi katika vikao vya Serikali,
hususan Baraza la Mawaziri, hivyo kupunguza changamoto ikiwemo kuchelewa kwa
taarifa, gharama kubwa za uchapaji na hatari ya upotevu wa taarifa muhimu.
Amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 11, 2024) wakati akifunga Mkutano wa
Kazi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa
Baraza La Mawaziri (e-CABINET), kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa hatua hiyo inatokana na jitihada na malengo ya Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusisitiza umuhimu wa Mawaziri na watumishi wa
umma kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika utendaji kazi,
“Matokeo ya mwaka 2023 ya ulinganifu baina ya nchi katika muktadha wa
Ukomavu wa Matumizi ya Teknolojia Serikalini (Government Technical Maturity
Index), nchi yetu ilishika nafasi ya tatu (3) ikilinganishwa na nchi nyingine
Barani Afrika. “Tunampongeza na kumtakia kila la kheri Rais Dkt. Samia aendelee
kubuni zaidi kwa manufaa ya Taifa letu . ”
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa mkutano huo kuhusu matumizi ya mfumo wa
kielektroniki wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za serikali katika
kuhakikisha kwamba Mawaziri na watumishi wa umma wanakuwa na ujuzi wa kisasa wa
uendeshaji wa shughuli za Serikali na utumishi kwa ujumla.
Kwa Upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewapongeza wataalam kutoka Wakala wa Serikali Mtandao kwa kufanikisha mafunzo hayo. “Tunaamini tumeelewa kwa kiwango kikubwa sana. ”
Waziri MkuuWaziri Mkuu
Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na mawaziri baada ya mkutano huo.
Baadhi ya mawaziri wakiwa kwenye mkutano huo.
0 Comments