Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa Zanzibar, huko Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
...............................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali za SMZ na SMT, zimeandaa mpango wa kuongeza vituo vya uchunguzi na
matibabu ya saratani kwa kutumia teknolojia ya nyuklia wenye thamani ya Euro
milioni 59.
Amesema, kupitia mpango huo, Serikali hizo zimedhamiria kuviongezea uwezo
vituo vya Ocean Road, Dar es Salaam, Bugando, Mwanza na kuanzisha vituo vipya
vinne kwa hospitali za Benjamini Mkapa Dodoma, KCMC Moshi, Mnazi Mmoja Zanzibar
na Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Samia Suluhu Hassan, alipofungua Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu
Tanzania (TAEC) kwa Zanzibar, huko Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini
Unguja.
Amesema, kukamilika kwa mpango huo kutaongeza huduma za matibabu ya
saratani kwa kutumia teknolojia ya nyuklia na Tanzania itakuwa na vituo sita
vya Serikali katika kanda zote muhimu nchini.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza ujenzi wa Ofisi na Maabara hiyo ni chachu
ya kuanza kwa ujenzi wa banki kwa ajili ya kuwekea vifaa vya nyuklia kwa
hospitali za Benjamini Mkapa Dodoma na KCMC Moshi.
Vilevile Dk.Mwinyi ameeleza kwa maendeleo ya kiteknolojia ya nishati ya
nyuklia pia yana uwezo wa kuchukua nafasi muhimu katika mchakato wa kuhama
kuelekea mfumo wa nishati usio na kaboni (Carbon) au hewa ukaa yanayoweza
kuzalisha umeme unaohitajika.
Halikadhalika , Dk. Mwinyi amezisisitiza Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kushirikiana pamoja na Wizara ya Nishati na wadau wengine kuandaa
mpango thabiti ili kuhakikisha Tanzania inaanza kunufaika na umeme wa nyuklia.
Kwa upande mwingine amesema lengo la ufunguzi wa ofisi hizo nchini ni
kuongeza usimamiaji na uendelezaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia
kwa wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akivuta pazia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa Zanzibar, huko Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Muonekano wa ofisi hiyo.
Muonekano wa ofisi hiyo kwa pande zote.
Furaha ikitamalaki baada ya ufunguzi wa fisi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo baada ya kufungua ofisi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia baada ya kufungua ofisi hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa ofisi hiyo.
0 Comments