Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI chini ya Mwneyekiti wake Mhe. Justin Nyamoga imeelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mapato ya ndani kwani ni miongoni mwa Halmashauri zenye mapato makubwa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jafari Wambura
Chege kwaniaba ya mwenyekiti wa kamati mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa
ghorofa sita wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Katika kata ya Mbagala kuu.
“kamati inaamini kuwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa ya Temeke
mnauwezo wa kukamilisha mradi huu kwa kutumia fedha za ndani na mkawa mfano kwa
Halmashauri nyingine zenye mapato makubwa nazo zikaweza kupata somo kupitia
Temeke”
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Nyamoga hiyo kwa
usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya marndeleo ambayo thamini ya fedha
inaonekana katika miradi hiyo.
Kamati hiyo ambayo imefanya ziara yake mkoani Dar es salaam katika Manispaa
ya Temeke imetembelea miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa shule ya sekondari
Magaya, ujenzi wa Bweni na bwalo katika shule ya sekondari Kibasira.
Pia kamati imetembelea na kukagua mradi wa mfereji wa Serengeti na Bwawa la
kuhifadhi maji ya mvua kwa Muda na mradi wa ujenzi wa Gorofa sita katika
hospitali ya Mbagala rangi Tatu katika kata ya Mbagala kuu.
ukaguzi wa ujenzi huo ukiendelea
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua mradi huo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea kutembelea mradi huo.
Muonekano wa mradi huo
Muonekano wa ujenzi wa mradi huo Mbgala.
Ukaguzi wa mradi huo ukiendelea
0 Comments