..............................
Na Mwandishi Wetu, Azerbaijan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Mkutano wa COP29 kulipa hadhi ya
kipekee suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mjadala wa
kuhamasisha upatikanaji fedha za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubia
Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa
Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji
wa Baku nchini Azerbaijan. Amesema Takriban watu milioni 900 barani Afrika bado
wanatumia nishati chafu katika kupika hivyo kusababisha ukataji miti, upotevu
wa sinki za kaboni na vifo kutokana na magonjwa yanayohusiana na moshi.
Makamu wa Rais amesema kutokana na umuhimu wa
suala hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan amekua kinara wa nishati safi Barani Afrika. Hadi sasa tayari amezindua
programu ya nishati safi ya kupikia ya kuwasaidia wanawake barani Afrika
(Pan-African Women Clean Support Programme) inayodhamiria kuhakikisha nishati
safi ya kupikia inatumika kama suluhu Barani, inayogharimu takriban dola
bilioni 4 kwa mwaka hadi kufikia 2030. Amesema hivi sasa Tanzania inatekeleza
mkakati utakaohakikisha upatikanaji wa nishati safi, salama na nafuu ya kupikia
kwa asilimia 80 ya kaya zote ifikapo 2034.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Mkutano wa
COP29 unapaswa kuhakikisha ahadi za fedha zilizotolewa zinatekelezwa kwa
kufanya maamuzi ambayo yatasaidia upatikanaji wa fedha kwa nchi kulingana na
udharura na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Aidha amesema kufanyika kwa mapitio ya malengo ya
kukusanya dola bilioni 100 iliyokubaliwa mwaka wa 2009 ni fursa ya kuleta
mabadiliko katika ufadhili wa mazingira kwa sababu yatakayokubaliwa yatatoa
taswira ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa miaka ijayo. Ameongeza
kwamba ufadhili wa mazingira ni wajibu na haki kama ilivyokubaliwa katika
Makataba wa Paris. Ametoa wito kwa COP29 kuimarisha mfuko wa Maafa ili
kuhakikisha fedha hizo zinaleta maana na kwenda sambamba na mafaniko
yaliyopatikana katika COP28 Dubai.
Makamu wa Rais amesema bado masoko ya biashara ya
kaboni hayajaainishwa vema ikiwa ni pamoja na ukosefu wa taarifa zinazowezesha
kushiriki kwa manufaa katika biashara hiyo hali inayopelekea nchi kukosa malipo
yanayostahili.
Aidha Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea
kuunga mkono juhudi za kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
pamoja na athari zake. Amesema kama yalivyo mataifa mengine yanayoendelea,
Tanzania pia inatumia rasilimali zake za ndani katika kutekeleza miradi ya
maendeleo inayochochea nishati safi, miundombinu ya usafirishaji rafiki kwa
mazingira, mifumo ya tahadhari iliyoboreshwa pamoja na udhibiti wa taka.
Amesema
Tanzania imedhamiria kulinda na kuhifadhi bahari na misitu ambapo ina jumla ya
eneo la hekta milioni 48.1 za hifadhi za misitu na makadirio ya uwezo wa
kuhifadhi kaboni sawa na 2% ya jumla
Mkutano ukiendelea
Muonekano wa mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo.
0 Comments