.......................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali
Mwinyi amesema maradhi yasioambukiza ni tatizo
linalokuwa na linalohitaji ushirikiano wa taasisi za ndani ya nchi na
kimataifa katika kulipatia njia Bora za
kukabiliana nalo.
Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo
alipozungumza na timu ya
Madaktari bingwa na Wataalamu wa
Maradhi yasioambukiza kutoka Geneva waliofika Ikulu kuonana na naye
tarehe 12 Novemba 2024.
Rais Dk,Mwinyi amefahamisha kuwa Zanzibar kama zilivo nchi nyengine duniani
imekuwa na wagonjwa wa wengi wa Maradhi
yasioambukiza wanaoongezeka kila mwaka hivyo inahitaji kuungwa mkono katika
juhudi zake za kudhibiti ongezeko la
wagonjwa wa aina hiyo.
Rais Dk, Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar inabeba mzigo mkubwa wa
Usafirishaji wa Wagonjwa kwenda nje ya
nchi kutibiwa magonjwa mbalimbali
ikwemo saratani hivyo suala la
kujengewa uwezo Wafanyakazi wa sekta ya
afya ni la umuhimu mkubwa.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesisitiza kwa Wizara ya afya kuendelea na
mchakato wa mazungumzo na timu hiyo ya Madaktari bingwa kwa dhamira ya kutafuta njia Bora utaalamu na
upatikanaji wa dawa za kutibu Maradhi yasioambukiza .
Rais Dk, Mwinyi amewahakikishia Madaktari bingwa hao kuwa Serikali ipo
tayari kushirikiana nao na kufanya kazi bega kwa bega kufanikisha lengo Lao la
kuja nchini kubaini changamoto na maeneo
ya Ushirikiano katika Sekta ya afya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na madaktari hao.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza na madaktari hao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na madaktari hao na viongozi wengine wa sekta ya afya.
0 Comments