VETA FURAHIKA YAIPONGEZA SMZ KUFADHILI WANAFUNZI 200 KIMASOMO

Subscribe Us

VETA FURAHIKA YAIPONGEZA SMZ KUFADHILI WANAFUNZI 200 KIMASOMO

Mkuu wa chuo cha Veta Furahika Dkt David Msuya akizungumza na waandishi wa habari.

 

Na Sophia Kingimali.

Mkuu wa chuo cha Veta Furahika Dkt David Msuya ameipongeza serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kufadhili wanafuzi 200 waliotoka katika kaya masikini kutoka Zanzibar kusoma katika chuo hicho.

Akizungumza leo Novemba 11,2024 jijini Dar es salaam amesema wamepokea wanafunzi hao kwenye kozi mbalimbali ikiwemo ushonaji na mapambo.

"Kipekee nimshukuru Rais Dkt Hussein Alli Mwinyi na serikali yake kwa ujumla kwa kuthamini vijana waliotoka katika mazingira magumu na kuona umuhimu wa kuwaendeleza kielimu ili waweze kujikwamua kimaisha na kuwaondoa kwenye vishawishi",Amesema Dkt Msuya.

Amesema mafunzo yanatolewa bure katika chuo hicho lengo likiwa kuhakikisha vijana wanatumia fursa hiyo kupata ujuzi ili waweze kujikwamua na kujiepusha vishawishi mitaani.

Sambamba na hayo Dkt Msuya amempongeza Mkurugenzi wa maendeleo ya jamii Zanzibar kwa kuonyesha ushirikiano na chuo hicho ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi na kujitegemea.

Pia, Dkt Msuya ametoa wito wa wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika chuo hicho kwani mafunzo ni bure na dirisha la usajili lipo wazi.

"Niwaombe wazazi na walezi pasipo kujali itikadi ya dini wala siasa wawalete watoto wapate ujuzi hapa elimu ni bure na tunakozi nyingi ambazo mtoto akitoka hapa ataweza kujiajili na kuajilika",Amesema.

Aidha ameongeza kuwa wameongeza kozi ya Tehama lakini pia wanatarajia kuanzisha kozi ya ufundi wa pikipiki ili kuhakikisha wanamgusa kila kijana ili waweze kujitegemea.

Kwa upande wake Mwanafunzi Safia Hamis Mwinyi ameishukuru Serikali ya mapinduzi kwa kuwafadhiri na anaamini elimu hiyo itaenda kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwaondoa kwenye utegemezi na kuweza kuwasaidia wazazi wao.

Wanafunzi wanaojifunza kushona nguo wakiwa katika mafunzo.
Wanafunzi wa ushonaji nguo wakiwa katika mafunzo.
Wanafunzi wa ususi wakiwa masomoni.
 

Post a Comment

0 Comments